JINSI YA KUTONGOZA MWANAMKE,KWA YULE ANAYEANZA - EDUSPORTSTZ

Latest

JINSI YA KUTONGOZA MWANAMKE,KWA YULE ANAYEANZA

JINSI YA KUTONGOZA MWANAMKE,KWA YULE ANAYEANZA

Kutongoza mwanamke si vigumu. Mwanamke ni kiumbe kama yeyote yule hapaswi kuogopewa.

Najua kuna wengi ambao hawajawahi kuaproach mwanamke na kumwambia matamanio yao. Hii inakubalika kabisa. Lakini hupaswi kamwe kuogopa mwanamke yeyote yule.

Nakumbuka kitambo kidogo mwanaume flani wa makamo kutoka Rwanda (miaka 35 huo wakati) alitutumia jumbe kwa panel yetu ya Nesi Mapenzi na akatuambia hajawahi kutongoza na kuwa anawaogopa wanawake.

Tulimfanyia mazoezi na sahizi ameoa. Kuna jambo ambalo tulisisitiza azingatie....nalo ni asiogope kitu. Na wakati anapoaproach mwanamke anapaswa kumdhalilisha ama kumshukisha hadhi.

Mbinu hii ya kumshusha hadhi mwanamke ama mtu yeyote huwa tunaitumia mara kwa mara bila kujijua. Na pindi utakapomshusha hadhi mtu basi unaweza kuondokewa na uoga papo hapo.

Mfano mzuri ni huu:-

Mara ngapi ushawahi kukutana na watu wanao omba omba pesa barabarani, nje ya maduka na ukawapuuza?
Hii ndio kushusha mtu hadhi. Akili yako unaifunga ili usimwonee huruma mtu kama yule anayeomba omba. Pindi utakapoanza kifikiria shida anazozipitia nyumbani kwake, njaa, ama ugonjwa alionao, basi bila shaka utampa pesa na zaidi unaweza kumpeleka hospitali ama kumtafutia makaazi ya kuishi.

Lakini kwa kuwa umemshusha hadhi hauoni shida zake.
Vivyo hivyo, mbona usimshushe hadhi mwanamke ili usione kuwa ni mrembo, anavutia ama atakukataa?

Narudia, jambo la kwanza nataka uelewe ya kwamba kutongoza si kazi ngumu, ni kama vile kuendesha baiskeli ama vile kuogelea. Mara ya kwanza unaweza kuona ni jambo gumu lakini ukifaulu mara ya kwanza basi hutoweza kushindwa kamwe.

 Wale marafiki zako ambao hakupiti mwanamke kabla hawajawatongoza walianza pale ulipo sasa, lakini baada ya muda wamekuwa mabingwa wa kutongoza.

Kabla hujaifahamu sanaa ya kutongoza naamini ya kuwa wewe ni mtu unayejiamini. Kujiamini wewe mwenyewe ni jambo muhimu ambalo linahitajika wakati wa kufanikisha kutongoza. Kama bado hujajijenga ili ujiamini wewe binafsi basi itakuwa vugumu kiasi kutekeleza swala la jinsi ya kutongoza.

1. Mpe Kipaumbele, atenshen(Attention)
Ushamtambulisha kuwa huyu ndie unayemzimia. Utafanya nini mpaka akunotice?

Kile cha kufanya hapa ni kumuangalia machoni mpaka aone aibu ya kukuangalia. Pia unaweza kucheza na mbinu ya kumuangalia halafu akitaka kukuangalia wewe unaangalia kando halafu unamuangalia papo hapo. Kufanya hivi kutakuwa kunavuta atenshen yake kutaka kujua mbona unapenda kumuangalia mara kwa mara.

NB: Usitumie mbinu hii mara kwa mara kwani unaweza kumuogopesha ama kukuona punguani.

2. Waguse kibahati mbaya
Iwapo huyo ambaye unamzimia ni mtu mnajuana, unaweza kumshika ama kugongana naye kibahati mbaya. Hii italeta atenshen kwenu wawili na utachukua nafasi ya kumuomba msamaha. Labda anaweza kukuuliza maswali ambapo unaweza kuendeleza na gumzo. Mfano unatembea halafu ukamgonga akaangusha vitabu vyake, ukamwambia samahani halafu akakujibu alikuwa anaenda kusoma maktabani, wewe ukamjibu kuwa ulikuwa umetoka huko sababu kuna joto jingi so unaelekea kusoma kwa uwanja. Halafu unamwomba kama anaweza kwenda na wewe kusoma pamoja.

Iwapo huwajui, kile unachotakiwa kufanya unaweza kumshika ama kugongana naye kibahati mbaya lakini usiongee kitu chochote. Mpe tabasamu halafu ujiondoe. Hii itamfanya kujiuliza maswali ya kwa nini umemfanya hivyo na anaweza kutaka kukujua zaidi ama kuuliza marafiki zake kukuhusu.

3. Ukiwa unaongea na yeye mpe dokezo kuhusu maisha yako
Iwapo umefaulu kuweza kupata kikao chake na chako, hakikisha wakati unapoongea mdokezee mambo mazuri ya kutoka kwako lakini usimuelezee kila kitu kukuhusu. Mfano unaweza kuwambia kuwa wewe ni msanii lakini usijieleze ni msanii wa aina gani. Kufanya hivi kutampa kiu cha kutaka kuongea na wewe siku nyingine ili kutaka kujua zaidi kukuhusu.

Pia wakati wa maongezi yenu hakikisha una nakili maneno yote ambayo huyo unayemzimia anapenda. Hii inaweza kuibua mada zaidi na zaidi wakati mtakapokutana mara nyingine.

4. Msogelee karibu na pale alipo
Wakati unapoongea na yeye kuwa jasiri wa kukaa karibu na pale alipo. Weka uoga kando na uonyeshe ujasiri wako wa kuongea na yeye akiwa karibu yako. Kufanya hivi utakuwa unaonyesha kuwa wewe unajiamini na kuwa hautikisiki. Wanawake hupenda sana  kuona mwanaume jasiri hivyo ukitumia mbinu hii kuna uwezekano mkubwa wa yeye kukupenda.

5. Leta tenshen ya kimapenzi
Pia unaweza kujaribu kufanya kumshika viganja vyake wakati unapoongea. Hapa kutaleta msisimko wa kimapenzi kati yenu. Mfano ikiwa unaongea na unayemzimia, unaweza kumuangalia kucha zake na kumwambia kuwa unazipenda. Atakuuliza kwa nini? Wewe mjibu kuwa kuna kitu ambacho kimekuvutia ambacho hujakielewa. Kama ataingiliana na huu mtego basi fanya kuushika mkono wake na kuanza kucheza na viganja vyake mkononi mwako. Pia unaweza kutumia mbinu ya kuleta ucheshi halafu mara moja au nyingine uwe unamgusa au kumdara mapajani au mkononi kuashiria kuwa jambo fulani linawachekesha. Hii moja kwa moja italeta tenshen ya kemia kati yenu.

NB: Kumbuka ya kuwa hii mbinu unaitumia kumfanya mwanamke akupende zaidi na wala haimaanishi ya kuwa itakusaidia kumpata kingono.

6. Mwangalie machoni
Hii ni mbinu ambayo imekuwa ikielezwa mara kwa mara ya kuwa lazima umuangalie mwanamke machoni wakati unajifunza jinsi ya kutongoza. Baadhi ya umuhimu wake ni:

 Unaweka atenshen yote kwa kitu kimoja, yaani unamwangalia umpendaye pasipo na kutatizwa na maswala mengine
 Inakupa mawazo ya haraka ya kufikiria wakati unapoongea
 Unamfanya yule unayeongea naye kukuona uko serious na mambo unayoongea.
 Kunapunguza wasiwasi
 Kunajenga tenshen ya kimapenzi kati yenu.

Mwisho: Ukihakikisha ya kuwa umefuata mbinu hizi kwa umakini, basi itakuwa rahisi kwako kuhakikisha ya kuwa umeweza kuteka hisia za yeyote yule ambaye umemzimia. Hapo ndipo unaweza kufunguka na kumwambia kuwa umemzimia na ungependa kuwa nayeye kama mpenzi wako. Kama bado unatashwishi ama uoga basi kuna kazi nzito inakungojea. 


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz