AKUKIFANYA WA AKIBA WEWE MPUNGUZE KABISA. KWENYE MAISHA YAKO.


Image result for ndoa
🍓Naomba  ujifunze hili iwapo Mtu anapokufanya wewe kama wa akiba, msaidie kupunguza akiba yake kwa kumuondoa kwenye maisha yako.

🍓Muda mwingine wewe nawe lazima uwe na ujasiri wa kuonyesha kuwa haujali, bila ya kuangalia ni kwa kiasi gani unajali!

🍓Kwa sababu inatokea muda mwingine mtu anakuona huna lolote wakati wewe unamuona ni kila kitu kwako!

🍓Kufanya hivyo sio kwamba unajisikia na unaringa, Hapana. bali ni kwamba unajiheshimu na zaidi unarudisha hadhi, thamani na utu wako!

🍓Usitarajie kuona mabadiliko yoyote chanya katika maisha kama bado unazungukwa na watu wenye mawazo hasi juu yako na wasioongeza thamani katika maisha yako!!

🍓Usiwape nafasi watu wa muda mfupi katika maisha yako. Fahamu thamani uliyonayo, na usikubali kupokea kidogo au kutopokea kabisa wakati unastahili kupokea makubwa zaidi ya hayo unayopewa!


Previous Post Next Post