ZIJUE SILAHA ZA KUDUMU PENZINI - EDUSPORTSTZ

Latest

ZIJUE SILAHA ZA KUDUMU PENZINI

ZIJUE SILAHA ZA KUDUMU PENZINI

UKIFANYA tathimini za kina, utagundua mapenzi ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Mapenzi ni kichocheo cha furaha, amani na mshikamano. Mapenzi yanaleta utulivu wa akili, yanatibu matamanio ya mwili.

Mapenzi yanaleta ufanisi wa kazi. Unapokuwa na ugomvi na mwenzi wako, ni dhahiri kwamba mambo yako mengine ikiwemo ya uzalishaji, yatayumba kama si kuharibika kabisa.

Hivyo basi, ukiyatathmini mapenzi kwa ujumla wake, yana faida nyingi, lakini leo nataka nikuongezee kitu kwenye ubongo wako, silaha ya kudumu penzini.

Uaminifu ni ngao ya mapenzi. Bila uaminifu hakuna mapenzi. Utampenda mtu sawa, lakini bila uaminifu, mapenzi ni kazi bure. Mtaishi, lakini mbeleni mtaishia kuachana. Mapenzi bila uaminifu ni sawa na gari linalokwenda bila dereva.

Litaenda safari, lakini itafika sehemu litaanguka. Uaminifu ni dira. Uaminifu unajenga tabia njema. Uaminifu ni silaha ya uhai wa penzi hivyo ni vyema mtu ukawa mwaminifu kwanza kabla hata ya kuingia kwenye mapenzi.

Uaminifu pia unaleta busara. Busara inawafanya wapendanao watatue matatizo yao kwa amani na utulivu. Busara inaepusha machafuko. Uaminifu ni msingi wa busara kama alivyosema muasisi wa madhehebu ya Buddha, Gautama Buddha;

“Honesty is the first chapter in the book of wisdom.”

Ukiingia kwenye mapenzi ukiwa huna uaminifu, ni sawasawa na kutega bomu ndani ya nyumba. Matunda ya kutokuwa na uaminifu siku zote ni usaliti. Usaliti unaleta maafa. Usaliti unatengeza chuki, usaliti unavunja uhusiano au ndoa.



Rafiki zangu, dunia ya leo sisi wote ni mashahidi. Tunashuhudia matukio mengi sana ya usaliti yanavyogharimu maisha ya watu. Usaliti ndiyo unafanya watu wavunje ndoa au wasisemezane maisha yao yote.

Watu wanauana kwa sababu tu, uaminifu umevunjwa. Ndiyo maana nikasema, uaminifu ni mhumu kuliko hata mapenzi. Wazungu wanasema; “In a relationship, trust is more impor tant than love. It will enhance your love.”

Uaminifu ndiyo unaoongeza au kujazia maana halisi ya mapenzi. Ni bora kabisa usiwe na mpenzi, lakini uwe mwaminifu. Maana, uaminifu una tija kubwa hata kwenye maisha ya kawaida.

Nikushirikishe pia na msemo huu wa Kingereza; “I trust you” is better than “I love you” because you may not always trust the person you love but you can always love the person you trust.”

Anamaanisha neno ‘nakuamini’, ni jema zaidi kuliko neno ‘nakupenda’ kwa sababu hatumuamini yule tunayempenda ila tunampenda yule tunayemuamini.

Uaminifu una manufaa makubwa kuliko kutokuwa nao. Uaminifu unakufanya uheshimike. Ukiwa muaminifu hata mawasiliano yako yatakuwa mazuri na mwenzi wako. Hamtagombanagombana. Mtaheshimiana. Mtakuwa kitu kimoja. Uaminifu unaanza na wewe, ukiwa mwaminifu, mwenzako naye atakuamini.

Jifunze kwa msemo huu; “When the trust is high, communication is easy, instant and effective.” (Kiwango cha uaminifu kikiwa juu, moja kwa moja mawasiliano yenu yatakuwa mazuri).


Ili maisha yaende, unashauriwa kujenga imani kubwa kwa mwenzako ili naye aweze kukuamini. Usiwe na shaka naye. Mwanafalsafa wa China, Laozi alisema; “He who does not trust enough will not be trusted.”

Anamaanisha, imani inaanza na wewe. Waamini wenzako ili na wao waweze kukuamini. Usiwe mtu wa shaka. Kama una shaka ni bora kutoingia kabisa kwenye uhusiano. Ishi na mtu unayemuamini.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz