πŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„MBINU 3⃣0⃣ ZA KUTEKA MAWAZO YA MWANAUMEπŸ‘„πŸ‘„NA KUWA MKE BORA KWA MMEOπŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„ - EDUSPORTSTZ

Latest

πŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„MBINU 3⃣0⃣ ZA KUTEKA MAWAZO YA MWANAUMEπŸ‘„πŸ‘„NA KUWA MKE BORA KWA MMEOπŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„πŸ‘„

UTAMUZAIDIAPP
πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—
1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima kama kuna jambo liko kinyume ongea nae taratibu mmeo atakuelewa,mke mwema uwa hapayukipayuki ovyo
2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako.
3). Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha.
4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.
5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo.
πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—
6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako kama mke na mama wa familia
7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe.sio kila kitu housegirl akusaidie utalia na mwewe kumbe hasidi ni wewe mwali,mpe huduma mmeo wewe mwwnyewe
8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na mpe matumaini huwez jua kesho atapata nini.uvumilivu kwenye ndoa ni jambo la msingi
9). Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo fanya jambo la busara na lenye faida kwa mmeo na familia
10). Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu mwali tena jambo hili zingatia kabisa.
πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—
11). Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.na usipoangalia unaweza kuibomoa nyumba yako ivi hivi.
12). Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. mwanaume anahitaji kuheshimiwa popote alipo
13). Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo subir mkiwa chumbani kama kuna kitu alikikosea mbele ya watoto mweleze taratibu
14). Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.
15). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo ni mbayasana ,kikulacho ki nguoni mwako
πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—
16). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa.
17). Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu.wewe na mmeo ndo waamuz wa mwisho
18). Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake.
19). Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.
20). Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu.
πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—
21). Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu
22). Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi jambo hili hukera sana wanaume,,ukiwana mmeo hutakiwi kuwa mvivu,hutakiwi kuwa mchafu.
23). Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula.chakula ni kitu muhimu sana na haswaa ujue mmeo anapendelea chakula kipi na kwa wakati upi
24). Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake.achana na tamaa ambazo huna uwezo nazo
25). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli.
πŸ’•πŸ’πŸ’“πŸ’—
26). Usiambatane na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa watqkupotosha,we umeolewa wenyewe hawajaolewa ni wazi hawawezi kukushauri lililojema kwenye ndoa yako
27). Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani wewe mwenyewe. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa.
28). Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri.
29). Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa.
30). Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako.Maombi hufungua mbingu na huleta baraka ndani ya ndoa,angalia ndoa zote zilizo imara na zenye mafanikio nyuma yake kuna mwanamke shujaa anaemwamini Mungu.

MKE MWEMA HUIJENGA NA KUILINDA NDOA YAKE MWENYEWE BALI MPUMBAVU HUIBOMOA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz