Kuna Watu Lazima Uachane Nao Ili Uweze Kupaa - EDUSPORTSTZ

Latest

Kuna Watu Lazima Uachane Nao Ili Uweze Kupaa

Kuna Watu Lazima Uachane Nao Ili Uweze Kupaa
Kuna Watu Lazima Uachane Nao Ili Uweze Kupaa

Kati ya ndege ambao Biblia imewatumia mara nyingi, nami siachi kujifunza kutoka kwake ni Tai. Life span ya Tai ni miaka 70, lakini anapofikia umri wa miaka 40, kucha zake ambazo ndizo huzitumia kwa ajili ya kubeba chakula chake huwa ndefu sana na kujikunja, hivyo hawezi kubeba tena chakula.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Mabawa yake nayo huwa mazito na kujikunja kifuani, hivyo anakuwa hana uwezo wa kupaa tena, kumbuka tai ndiye ndege mwenye uwezo wa kupaa masafa marefu kuliko ndege yoyote chini ya dunia.

Mdomo wake pia huwa mrefu, butu na kunikunja, hivyo hawezi pia kuutumia kwa ajili ya kazi zake kama kujenga kiota chake au kuchukua chakula.

Tai anapofikia hatua hii, huwa anakuwa amebaki na options mbili achague kufa au aamue kukubali kupitia mchakato wa mabadiliko ambao huwa ni wa maumivu sana na inamchukua siku nyingi kadhaa kujitenga na kila kitu maana hupaa hadi kwenye kilele cha mlima mrefu sana na huko huanza process za mabadiliko ya mwili wake.

Kwanza huanza kwa kuanza kujipiga mdomo wake kwenye mwamba mpaka utakapotoka wote, kumbuka ni maumivu makubwa sana anayapata, lakini lazima afanye hivyo, maana anataka kuja kupaa viwango vya juu sana na mdomo uliozeeka na kujikunja utamzuia kupata chakula na kufanya shughuli zake.

Baada ya kuuondoa, hukaa na kusubiria uote upya kwa siku kadhaa na baada ya hapo huanza kuchomoa kucha zilizozeeka na kujikunja na mwisho kabisa huanza kung’oa mabawa yale yaliyochoka. Baada ya hapo huzaliwa upya na kila kitu kuwa upya na huweza kuishi miaka 30 iliyobaki na kupaa viwango vya juu sana na masafa marefu.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Katika maisha kuna nyakati unakuta huwezi kwenda viwango vya juu, kila malengo unayoyapanga hayapangiki wala kufanikiwa, unajiuliza tatizo ni nini mbona kila kitu cha kukufanya ufanikiwe unacho?

Hebu jaribu kuangalia watu unaoambatana nao, je, wanakufanya kuwa bora au ni watu wanaokuwa kama kucha za tai zilizorefuka na kujikunja au hao rafiki ni mdomo wa tai uliokuwa butu na kukuzuia usiweze kufanya shughuli zako au rafiki huyo ni mabawa ya Tai yaliyokuwa mazito na kukuzuia kupaa viwango vya juu na masafa marefu?

Unapokuwa unasafiri na ndege, kuna watu wengi wanaweza kukusindikiza mpaka uwanja wa ndege, lakini unapotakiwa kuingia ndani kukaguliwa, ni wewe tu unayeingia. Aliyekusindikiza huwenda akawa mmeo au mkeo au mzazi au mtoto, lakini lazima tu uwaage na kuwaacha mle ndani unaingia wewe tu.

Huwa ni kitendo cha huzuni, lakini haina budi kuwaaga maana wewe tu ndiye uliyelipa garama ya kusafiri na ndege na unajua maumivu unayoyapata kulipia ndege halafu ikuache kwa kuchelewa kufika uwanja wa ndege.

Wewe ndiye unayejua gharama ya maono yako, wewe ndiye uliyelipa gharama ya kile unachotaka kukiona kikitokea kwenye maisha yako. Kuna wengine hawawezi kukuelewa. Itakuwa ni ujinga wa hali ya juu kulazimisha usafiri na watu wote waliokusindikiza uwanja wa ndege wakati wao hawajalipia tiketi, utakuwa unataka na wewe uachwe na ndege.

Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya 13 yote, utaona habari za Ibrahimu na ndugu yake Lutu walikuwa wakigombana kwa sababu wote walikuwa na mifugo mingi na eneo la malisho ya wanyama lilikuwa dogo.

Ni baada ya Ibrahimu kuamua kutengana na Lutu na kumwambia ajichagulie anapoona ni pazuri, Mungu alimfungua macho na kumuonesha eneo zuri zaidi ya lile walilokuwa wanagombania.


Biblia inasema katika Mwanzo 13:14-15; “Bwana akamwambia Abrahamu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa Kaskazini na wa Kusini na wa Mashariki na wa Magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.”

Kumbe kuna watu ukiwa nao, shirika hutaweza kuona fursa mpya mbele yako. Kuna mawazo ya biashara hutayaona japokuwa yapo. Kuna masoko hutayaona japokuwa yapo. Lakini muda mnaachana tu, unaanza kuona kufanikiwa, unaanza kupata mawazo mapya, unaanza kuona kuinuliwa na kupaa viwango vya juu.

Kuna watu lazima tuachane nao ili tuweze kupaa viwango vya juu, maana kuna watu uko nao kila ukijaribu kufanya jambo wanakukatisha tamaa kuwa huwezi.

Muda mwingi wao huongelea kushindwa. Ni watu wa kujadili maisha ya watu. Hawajawahi kukusapoti jambo lolote zaidi ya kukushusha kila unapojaribu kupaa viwango vya juu, wakiona umefanikiwa kidogo wanaumia mioyo, yaani hawafurahii mafanikio yako hata siku moja.

Watu wa namna hii huna budi uachane nao. Hii ni njia ambayo inaweza kukuletea maumivu lakini kwa sababu unataka kwenda viwango vingine na kupaa juu sana, ni lazima tu uwapunguze au kuwaondoa kabisa katika safari ya mafanikio yako.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Rafiki usiwe mabawa, kucha na mdomo uliozeeka kwangu kama mabawa ya tai na kunizuia kupaa masafa marefu, maana hakuna namna nitakuondoa mwilini mwangu. Na mimi kama pia nakuzuia kupaa, niondoe mwilini mwako.

Je, wewe unawasaidia wenzako kuinuliwa na kufanikiwa au umekuwa sababu ya kuwazuia, kuwakatisha tamaa na kuwasema vibaya? Je, umekuwa sababu ya mwenzako uliye naye kuona fursa na mafanikio au umekuwa kauzibe hakuna lolote analiona mbele yake zaidi ya kuona kushindwa? Jichunguze na ujifanyie tathimini.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz