WANAUME KULALA USINGIZI BAADA YA TENDO LA NDOA, NINI CHANZO


Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.

Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.

Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.

"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.

“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.

Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post