USISEME HAKUNA WANAUME WA KUOA AMA WANAWAKE WA KUOLEWA - EDUSPORTSTZ

Latest

USISEME HAKUNA WANAUME WA KUOA AMA WANAWAKE WA KUOLEWA


Jamii tunayoishi imejaa watu tuliokata tamaa na mbaya zaidi tuna wakatisha na wengine tamaa juu ya suala la kupata mwenza wa ndoa na maisha ya ndoa kwa ujumla.
Unakuta wanaume tunasema hakuna wanawake wanaofaa kuolewa labda kama kumpa wa kuwapa mimba ili kupata watoto tu.tuna dai wanawake wanapenda pesa tu.
wanawake nao wanataka wanaume wa kuwapa mimba tu.Hawataki kuolewa kwa kuamini ndoa ni ngumu na wanaume wote ni sawa,hakuna mwema yaani wote hawafai.
Nadhani wengi wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini wanasikia habari mbaya tu.Yaani ndoa zote zinazofungwa kila uchwao alafu wao wanasema hakuna waoaji ama waolewaji !!!???
.Yaani wanaangalia ndoa zenye zilizoharibika badala ya ndoa zilizosimama na kumpa Mungu utukufu.
Swali la kujiuliza ni kwamba, ukiangalia mabinti,vijana/wanawake ama wanaume unaona nini? Unaona mtu anayefaa kuwa mume ama mke? Au unaona watu kama miti tu?.
Wakati wengine wakiona fursa ya wake wema na waume wenye akili katikati ya mazingira yaleyale unayoishi wewe,kwako ni tofauti maana una mawazo hasi.
Kama hauwezi kubadilisha mawazo na mtazamo wako utaishia kuona wengine wakifunga ndoa na kufurahia maisha yao.Kumbi kibao za sherehe zimejaa booking za watu wanaotaka kufunga ndoa kila leo alafu wewe unasema hakuna wa kuoa ama kuolewa?!!!!
Unasema hata wakioana hawadumu pasipo kujua hao ni wale wasiojua kusudi la ndoa na waliochangua kushindwa.
Mungu atupe ndoa yenye amani na upendo kwa wale ambao hatuja ingia ktk Ndoa.
Ndoa ni muhimu ukimpata mtu sahihi. Omba uliye nae asibadilike.
Tunataman KUOA wengine KUOLEWA ila mtihan kumjua mukwel
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz