TOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME KWENYE SUALA LA MAPENZI I HII - EDUSPORTSTZ

Latest

TOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME KWENYE SUALA LA MAPENZI I HII

Tofauti kati ya wanawake na wanaume nikuwa wanawake wanaamini kuwa ni kazi ya wanaume kuwafurahisha wakati wanaume wanaamini kuwa ni kazi yao wenyewe kujifurahisha. Labda nikupe mfano mmoja, mwanaume ambaye anakunywa pombe hawezi kuacha pombe kwakua ameoa, ataendelea kutoka na marafiki zake, kunywa na kufurahia bila kujali kama mke wake anafurahia au la. Lakini mwanamke ambaye anakunywa pombe ni mara chache sana anaweza kutoka na kwenda kunywa akamuacha mume ndani na pombe ikamshuka vizuri.
Najua mfano huu si sahihi sana lakini nilitaka wanawake muelewe kuwa, kuna wakati ni lazima utafuite kitu cha kukupa furaha wewe peke yako, ambacho hakimuhiaji mwanaume. Hata kama kutokana na malezi kwamba huwezi kutoka kunywa na kumuacha mwanaume ndani, lakini kuna mambo mengine mengi ya kujifanyia, wewe mwanaume katoka na marafiki, labda tuseme anarudi saa nane usiku, hajali kama ana mke, hajali kama unafuraha, hajali chochote kile.
Sasa sisemi na wewe utoke kwani haitakua ndoa tena yatakua mashindano lakini badala ya kukaa kuanzia saa mbili usiku watoto wamelala, huli chakula na hulali mpaka saa nane usiku aje ndiyo mle pamoja hembu hata lala. Kula chakula chako vizuri tena kishuke, na muambie kabisa kuwa mimi siwezi kukusubiri mpaka saa nane ndiyo tule, kula lala, akierudi kipo kwenye hotpot ale asile ni tumbo lake.
Mtu kakurudia saa nane eti une neng’eneng’eka kuwa hajala chakula kana kwamba huko alikua anakusanya njaa tu ili aje kula. Badala ya kuvumilia kila siku, tafuta kazi, kwamba mwanaume anakuboa kila siku, badala ya kugombana naye kwanini anakuja saa nane usiku, gombana naye kwanini hataki ufanye kazi? Gombana naye kwa vitu ambavyo vitakujenga, na hapa naomba nifafanue, kama unataka furaha ya kweli ni lazima uweze kujitegemea katika kuitengeneza.
Kuna mambo mengi ambayo mwanamke unaweza kujifanyia, kama ukiilzamisha akili yako, ukaiambia kuwa furaha yangu haimtegemei huyu mtu basi pombe zake, wanawake zake hawatakusumbua! Sanasana utakua na ujasiri wa kusema “Sikuamini tutumie kinga!” Utakua na ujasiri huo kwakua utakua na kazi na unajipenda wewe. Soma kitabu change cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” sehemu ya nne. Bei yake ni shilingi elifu kumi tu, kukipata unalipia kwa M-Pes No. 0742-381-155 au Tigo Pesa Bo, 0657-552-222 na kitabu unatumiwa kwa njia ya Whatsapp, Email au Facebook.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz