enzi ni pale unapokua na mwenza ambaye anakufahamu kuliko hata unavyojifahamu, utamu wake upo pale ambapo mwenza wako anajua ni kitu gani akikufanyia kitakupa furaha na kitu gani hapaswi kukufanyia kabisa kwani kitakuumiza au kukuharibia mood. Unapokua na mtu wa namna hii basi ni vigumu sana kuyakinahi mapenzi!
Wanaume wengi hawafahamu mambo ambayo Wanawake hupenda, hii ni kwasababu akili za wanaume mara nyingi hazipo katika vitu vidogo vidogo, hivi ni vitu ambavyo kwa wanawake ni vikubwa na kama unataka mwanamke akugande basi ni lazima kumfanyia vitu hivi. Si kufanya tu, hapana kufanya bila kuambiwa, bila kuwa na ulazima wa mwanamke kusema napenda kitu flani!
(1) Kumtoa Out; Unaweza kuwa ndiyo umekutana naye au umekaa naye kwenye mahusiano muda mrefu, lakini hata ni mke wako. Jua kuwa anapenda umtoe out tena bila ya yeye kukuambia au kukuomba. Inaboa na haina raha kama akikuomba, kama mwanaume nilazima uwe na utaratibu huu kwani wanawake wote wanapenda, hata huyo wakwako unayemuona wa kijijini anapenda.
Kama ni mpenzi wako out sio kumpeleka Geto kwako kila siku inaboa, nilazima mbadilishe mazingira ya mechi, hata kama ni mkeo. Wanawake hata hawataki gharama kwamba ni lazima umpeleke sehemu ya ghali sana, hapana kwake cha muhimu ni kule kutoka out kuongozana na wewe kuliko hata gharama mtakazo tumia, hivyo kama unataka we na furaha mtoe.
(2) Kusifiwa: Hakuna mwanamke ambaye hapendi kusifiwa na ukisikia anasema hapendi basi jua kalelewa vibaya, jua hajalelewa kikike kiasi kwamba amesahau namna ya kuwa mwanamke. Mwanamke hatumii masaa mawili katika kioo kujiremba kwakua tu anapenda marangi usoni, hapana anapenda kuonekana na anataka kusifiwa.
Inakua tamu zaidi kama ukimuona na kumsifia tena si kwa kumuambia umpendeza hapana kwa kumuambia umependeza hasa namna nyewele zilivyokaa, suruali au ulivyo mechisha, kwa kifupi usifie kitu halisi. Unapokua humsifii anapopika chakula kizuri, namna anavyolea watoto, muonekano wake basi unamfanya kujiona hana thamani na siku akipata mtu wa kumsifia hata kama ni jirani tu basi atampenda zaidi ya anavyokupenda.
(3) Kuachana Na Tabia Za Kibachela; Labda ni mke au mpenzi, tunajua wanaume mabachela wengi wao hawapendi kufua, kupika kuosha vyombo na wako rafurafu, hizo ndiyo tabia za kibachela. Bila kukuambia mpenzi wako atafurahi kama utaanza kubadilika kwaajili yake na kuziacha taratibu, hata kama si kila siku lakini umsaidie kufanya baadhi ya vitu hapo nyumbani au wewe kujirekebisha kwaajili yake.
(4) Muda Wa Peke Yake Bila Wewe; Kama ambavyo sisi wanaume tunapenda kuwa peke yetu, wakati mwingine kutoka kutuliza mawazo labda na marafiki bila kubughudhiwa na familia, bila kuwaza kuhusu mke na kuchangamsha kichwa, hata wanawake hupenda hivyo. Yeye kuwa mke au mpenzi wako haimaanishi umchunge na kutaka kuwa naye kila wakati, hapana, kama binadamu anahitaji kuwa peke yake.
Kuna wakati anahitaji kutoka na marafiki zake, kutoka mwenyewe na kupata muda wa kupumzika mwenyewe. Muda wa kutafakari mambo yake bila wewe, kua katika mahusiano haimaanishi kuwa pamoja kila wakati. Ni vizuri kumpa muda wa kuwa mbali na wewe, umruhusu akumiss, umruhusu kufanya mambo bila kuwa na wewe, anapenda sana hiyo nafasi na anataka kuipata bila kuiomba.
(5) Kupigiwa Simu Na Kutumiwa Meseji Nzuri; Kuna wanaume ambao wakishapendwa hujisahau, husahau kupiga simu mpaka pale wanapohitaji kitu flani, husahau kusalimia asubuhi. Lakini kubwa hawatumi meseji kabisa, hapana katika mapenzi meseji ni za lazima. Wanawake hupenda kutumiwa meseji nzuri, umtumie na kumsifia, meseji ambayo atakuja kuisoma baadaya na kucheka au kutabasamu akisema flani ananipenda.
Hapa sizungumzii zile meseji za kumuambia fanya kitu flani au kumuulizia kuhusu watoto hapana. Mtumie meseji muambie namna unavyompenda, namna anavyokufanya ujisikie na namna unavyofurahia mwili wake. Muambie namna unvayomuwaza kwa wakati huo. Kwa mfano “Nimekaa hapa ofisini sina mood kabisa lakini nikaanza kukukumuka kila kitu kikawa sawa, nimekumbuka kale kasauti kako kachumbani sasa kazi zinaenda!”
(6) Kukumbuka Matukio Yake Muhimu; Hivi ni vitu ambavyo mara nyingi wanaume hatuviangalii, lakini kukumbuka vitu kama siku yake ya kuzaliwa, siku mliyokutana, kukumbuka siku ambayo alipata kitu flani na matukio yake muhimu kutamfanya mwanamke kuchanganyikiwa zaidi juu yako. Kwamba unapokumbuka na kumnunulia kazawadi inamfanya akuone wewe ni wapekee kwani mara nyingi wanawake hawategemei wanaume kukumbuka mambo kama hayo.
(7) Kuwakumbuka Ndugu Zake; Mara nyingi katika mahusiano hasa katika ndoa ndugu wa mume ndiyo hupewa kipaumbele, huonekana kama ndiyo wenye familia na ninadra sana ndugu wa mke kukumbukwa. Hapa simaanishi katika kusaidia tu hapana, bali hata katika salamu, hembu muulizie kuhusu ndugu zake, alikuambia Mama yake anaumwa kumbuka na ulizia.
Umekaa muda mrefu hujaenda kusalimia kwao usisubiri akuammbie mpigie Mama simu au nenda kusalimia, hapana kumbuka na siku moja ukimuambia “Mama anakusalimia” basi asiwe ni Mama yako bali Mama yake. Unapokua unawakumbuka na kuwajali ndugu zake unakua umemuonyesha upendo kwani wale ni watu aliokua nao anawapenda kama wewe unavyowapenda ndugu zako onyesha kuwajali.
(8) Kumfanyia Shopping; Hapa sizungumzii kutoa mamilioni kwenda Mlimani City, kama unayo ni kitu kizuri kutoa lakini moja ya vitu ambavyo vitamfanya mke wako au mpenzi wako kujiona wa thamani ni wewe kumnunulia nguo kama zawadi, inaweza kuwa hana ni underwear lakini ataivaa akisema kuwa nimenunuliwa na mume au mpenzi wangu.
Kumbuka inawezekana unampa hela lakini husikia raha zaidi kama utaongozana naye wakati anaenda kununua na ukamchagulia wewe lakini raha huwa raha zaidi pale ambapo wewe mwenyewe utajiongeza, ukajua saizi yake na kwenda kumnunulia kama zawadi. Hata kama ana pesa kiasi gani lakini mwanamke anapenda zawadi na zawadi ya nguo (au kitu cha kuvaa) ina umuhimu sana itawaunganisha kwani kila atakapokua anaivaa atakumbuka siku uliyompa.
(9) Kushirikishwa Na Kusikilizwa; Kiasilia wanaume tunajiona tuko juu, tunadhani wana akili zaidi kuliko wanawake, hii si kweli kuna wanawake wengi tu majembe kuliko wanaume. Lakini hii si ishu hata kama ni kweli umemzidi mke wako kwa kila kitu atajisikia raha sana kama kama utakua umemshirikisha, usifanye mambo kimya kimya tena hasa kama ni mke wako, kumbuka yeye ndiyo Mama au atakua Mama wa watoto wako.
Nilazima umshitikishe, usikilize mawazo yake hata kama hutachukua lakini umpe nafasi ya kuongea na kama ukiyakataa uyakatae kistaarabu. Hakuna uanaume katika kumdharau mke au mpenzi wako halafu wakati hupo huo unajifanya kumpenda Mama yako, kumbuka hata Mama yako alikua mke wa Baba yako, ingawa sasa hivi unamuona ana maana upo wakati ambao wanao watamuona mkeo naye anamaana, mheshimu anafurahi sana kusikilizwa na kuthaminiwa.
(10) Kuambiwa Nakupenda; Kibongo bongo haya mambo ni kama hayapo lakini kumuambia unampenda ni kitu cha maana sana na kinamfanya mwanamke kukupenda zaidi na kuwa na furaha sana. Unapaswa kukumbuka kuwa katika mahusiano jinsi muda unavyozidi kwenda ndivyo ambavyo mwanamke hujiona kazeeka na hujiona kama hapendwi tena, kwa maana hiyo kuwa na wasiwasi na kukosa furaha.
Sasa ni kazi yako wewe mwanaume kumuonyesha kuwa si kweli, kumuonyesha kuwa hujamzoea na yeye ndiyo yule binti ambaye mlikutana miaka kadhaa iliyopita. Fanya hivyo kwa kumkumbusha mara kwa mara kuwa unampenda, kutambua thamani yake na kumuambia hujui kama maisha yako yangekuaje bila yeye, usiseme tu muonyeshe, kila kwamamke hupenda kuambiwa anapendwa bila kuomba kuambiwa.
No comments:
Post a Comment