KWA WADADA WANAOPENDA KUHAMIA KWA WACHUMBA KABLA YA NDOA SOMA HAPA - EDUSPORTSTZ

Latest

KWA WADADA WANAOPENDA KUHAMIA KWA WACHUMBA KABLA YA NDOA SOMA HAPA

Image result for Mwanaume anakuambia anaishi peke yake,

NATAKA NIONGEE NA HAWA WANAWAKE HAWA AMBAO WAMETONGOZWA SIKU YA KWANZA YA TATU WAMEAMIA KWA MWANAUME
TUNAJIULIZA KWANINI WANAWAKE SIKU HIZI TUNADHARAULIWA SANA, SABABU KUBWA NI TUNASABABISHA SISI WENYEWE, WANAWAKE TUNAJIRAHISISHA SANA KWA WANAUME MPAKA WANATUDHARAU
MWANAUME AKIKUCHEKEA SIKU MOJA YA PILI KAKULAZA KITANDANI, BORA BASI UWE HATA ULIKUA UNAMJUA SIKU NYINGI UNAMJUA NI WA AINA GANI, LAKINI WALA SHOGA YULE KIJANA HUMJUI KAMA MCHAWI, KAMA MWIZI WEWE ILIMRADI TU KAKUCHEKEA USHAVUA NGUO
MWANAMKE UTAMKUTA MZURI MASIKINI KAHAMIA KWA MWANAUME MWAKA SIJUI WANGAPI HUU NDOA HAMNA UNAANZA KULALAMIKA SASA ATAKUOAJE NA WEWE UMEJIHAMISHIA HUKO NA UNAFANYA KAZI KAMA ZA MKE????
MBAYA ZAIDI UTAKUTA MTU UMEHAMIA KWA MWANAUME MWANAUME MWENYEWE HAELEWEKI MBELE WAPI NYUMA WAPI, WA MOTO AU WA BARIDI, YEYE KUTWA WA VUGUVUGU UNATESWA NA KUNYANYASWA NA VITUKO KIBAO LAKINI UMENG'ANG'ANA TU ETI UONEKANE WIFE MATERIAL...HALAFU AKISHAKUTUMIA ANAKUACHA ANAOA MWENGINE
MWANAMKE UNAJIPA MOYO ETI NAKABA MPAKA PENALTY UNAWEZA KUMKABA MWANAUME WEWE, MWANAUME HACHUNGWI KWA TAARIFA YAKO AKIAMUA LAKE KAAMUA AKIAMUA KUTULIA NA KUKUA WEWE ATAKUOA NA AKIAMUA KUKUTUMIA ATAKUTUMIA NA KUKUCHAKAZA NA MWISHO KUKUACHA AKAOE CHOMBO KIPYA
HALAFU KINACHONIUDHI MIMI YANI SAA ZINGINE SIJUI HUA HATUFIKIRII MWANAMKE UMEHAMIA KWA BWANA HATA HANA DALILI YA KUKUOA UNAENDA KUJITAFUTISHA MIMBA UNAJIPACHIKA UNATEGEMEA SIJUI ATAKUOA..YANI MIMI HII TABIA INANIKERA MIMI KWANI UKITUMIA UZAZI WA MPANGO JE, AMA CALENDER UKAJISTAHI MTOTO WA KIKE MIMBA UKAIBEBEA NDANI YA NDOA UTAPATA HASARA GANI, WATOTO WOTE WATAMU LAKINI WANAKUA WATAMU ZAIDI WAKIBEBWA NA KULELEWA NA WAZAZI WOTE WAWILI WALIOBARIKIWA KWENYE NDOA
KWELI SAA ZINGINE KUNA WANAUME WA KWELI UNAHAMIA MUDA MCHACHE TU WANAKUOA ILA WENGI NI WAONGO JAMANI UNAKAA MIAKA MIWILI MITATU HUJAOLEWA NA WEWE BADO TUU UMEKAA UNAJIPA MOYO ETI TUNASOMANA HICHO MNACHOSOMANA NYIE MIAKA MITATU NI KIPI HASWA AMBACHO HAKIISHI
WENGINE MPAKA WANAISHIA KUSAVE NA HAO WANAUME WANANUNUA MAGARI PAMOJA NA KUJENGA NYUMBA HALAFU MWANAUME ANAKUDANGANYA JINA ANAWEKA LAKE ETI KWENYE NDOA BABA NDIO KILA KITU BAADAE UNAACHWA ANAOA MWANAMKE MWENGINE ANAKUJA KUFAIDI JASHO LAKO KIULAINI..UNALIA OOHHH NINAMKOSI YULE MWANAMKE KANILOGA NIACHIKE AKULOGE NANI WEWE HUJATUMIA AKILI VIZURI MWANAUME KAKUONA SIO WOFE MATERIAL KAKUACHA KAOA MKE..UTABAKI HIVYOHIVYO KULALAMIKA UMELOGWA
KUNA DADA MMOJA HIVIHIVI ZA HAMIAHAMIA ALIKUA NA MWANAUME WAKE WAKAAMUA WAKAE PAMOJA BILA NDOA
MIAKA IKAENDA MWANAMKE YULE ALIKUA MCHAKAKARIKAJI SANA AKAWA ANAPATA PESA ZAKE ANACHANGANYA NA MWANAUME WANAJENGA WANAJINYIMA NA KUJENGA WENYEWE MPAKA NYUMBA IKAISHA..WAKAHAMIA
WAKATI WANAKAA HUKO MWANAMKE AKABEBA MIMBA AKAJIFUNGUA NA WAKATI WOTE HUO HAKUNA NDOA, BAADA YA KUJIFUNGUA WAKAENDELEA NA MAISHA YAO HUKU NA KULE WAKAANZA KUJENGA NYUMBA YA PILI IKAKAMILIKA HII YA KWANZA WAKAPANGISHA WAKAAMIA KWENYE YA PILI TABATA HUKO
BADO HAWAJAOANA, MAISHA YAKASONGA MTOTO NAYE AKAKUA YULE BABA NI MTU WA TANGA AKASAFIRI SIKU MOJA KWENDA KIJIJINI KWAO WAKATI YUPO KIJIJINI AKAMUONA MWANAMKE HUKO AKAMPENDA KUMCHUNGUZA FAMILIA WAKASEMA HUYU MTOTO NI MZURI SANA ANAHESHIMA ANAFAA KUA MKEO
MIPANGO IKAFANYIKA YA YULE BABA KUOA YULE MWANAMKE, AKARUDI KUMTAARIFU MAMA MTOTO WAKE KWAMBA NYUMBANI WAMEMTAFUTIA MKE WA KUOA KWAHIYO AMEAMUA KUOA
YULE DADA ALIDONDOKA KWA PRESHA, AKAAMKA KUJIKUTA HOSPITAL KUTIBIWA AKAPONA NDIO AKAANZA KAMA KUCHANGANYIKIWA, NDUGU ZAKE WAKAMCHUKUA NA KUMRUDISHA KWAO ILALA ILI WAMTIBIE APONE MAANA ALIANZA KUCHANGANYIKIWA
AKAKA KWAO HUKU MWANAUME AKAOA AKAMLETA YULE MWANAMKE NYUMBANI KWAKE PALE ALIPOKUA AKIISHI NA YULE MAMA MTOTO WAKE, KULA HABARI ZIKAMFIKIA MAMA MTOTO WAKE AKAWA ANAUMIA LAKINI WAZAZI WAKE WALIMSII KAA MWANANGU UTULIE UPONE KWANZA AFYA YAKO SIO NZURI, MALI UTATAFUTA LAKINI UKIFA MWANAO ATAPATA TABU
BASI YULE DADA WAZAZI WAKE WAKAHANGAIKA NAYE MPAKA KUPONA, KUANZA TENA KUISHI PALE NYUMBANI KWAO MAANA ALIKUA HANA PA KWENDA KWA MUDA HUO, AKAWAOMBA NDUGU ZAKE WAKAMCHUKULIE VITU VYAKE KWA BABA MTOTO WAKE WAKAWA WAMEMALIZANA HIVYO
MAISHA YAKAENDELEA KULE YULE BABA NA MKEWE WAKAPATA MTOTO MMOJA WAKASONGA, HIVYOHIVYO SIKU ZINAKATIKA MAISHA YANAENDA LAKINI NDANI YA MOYO WA YULE BABA HAKUA NA AMANI BAADA YA KUSIKIA YALIYOMTOKEA MAMA MTOTO WAKE KUUMWA KISA YEYE
BASI SIKUA AKATAFUTA MUDA AKAENDA NYUMBANI KWA MAMA MTOTO WAKE ANAPOISHI NA WAZAZI WAKE KULE ILALA AKAENDA KUOMBA MSAMAHA KWA YOTE NA KUMWAMBIA KATIKA ILE NYUMBA WANAYOPANGISHA BASI ACHUKUE VYUMBA VIWILI VYA WAPANGAJI ILI IWE HELA YA KUMSAIDIA KULEA MWANAE
BASI YULE BABA AKAONDOKA NA MAISHA YAKAWA HIVYO YULE MAMA AKAWA ANAVYUMBA VYAKE WIWILI KULE WAPANGAJI WANAMLIA HELA YEYE MAISHA YANASONGA, MPAKA AKAPONA KABISA NA KUAMUA SASA ANATAKA KWENDA KUPANGA ILI AANZE UPYA MAISHA YAKE NA MWANAE..AKAONDOKA KWAO NA KWENDA KUPANGA HUKOHUKO ILALA
BASI MAISHA YAKAENDA, YULE BABA AKAWA ANAWASILIANA NA HUYU MAMA KUTAKA KUJUA MWANAE ANAENDELEAJE, YULE MAMA AKAWA ANAMRUHUSU KUJA KUMUONA MWANAE BABA AKAWA ANAENDA NA KUMUHUDUMIA ANAACHA HELA ZA MATUMIZI PALE, MTOTO ANASOMA SHULE YA KUELEWEKA MAHUSIANO YAO YAKAWA MAZURI SASA
KULE MKEWE AKASIKIA KWAMBA MUMEWE ANAMUHUDUMIA YULE MAMA NA MWANAE AKAWA MKALI SANA KWA MUMEWE, AKAWA HATAKI HATA HUYO MAMA AKANYAGE PALE KWENYE NYUMBA YAO WALA MWANAE BASI IKAWA VITA KUBWA SANA
SIKU ZIKAENDELEA SASA IKAFIKA MPAKA YULE BABA AKAWA ANAENDA KWA MAMA MTOTO WAKE MARA NYINGI YANI AKAZOELEKA KULE KAMA MUME WA YULE DADA, NA MPAKA KUFIKIA HIVYO HUJUE NA MZIGO ALIKUA ANAKULA, SIDHANI KAMA WALIKUA WANAONGEA TU MUDA WOTE KUHUSU MTOTO
SASA WIKI MBILI ZILIZOPITA YULE BABA SIKU HIYO KATOKA ZAKE KAZINI AKAENDA ILALA KWA YULE MAMA MTOTO WAKE KUFIKA PALE AKAMWAMBIA MAMA RAHMA JAMES LEO SIKISIKII VIZURI KABISA, YANI NAJISIKIA KUUMWA YULE MAMA AKAMWAMBIA BASI NGOJA NIKUPE CHAKULA UOGE UPUMZIKE, IKAWA HIVYO
ILA YULE BABA ALISHINDWA KUPUMZIKA KWA VILE ALIKUA ANAJISIKIA VIBAYA BASI YULE MAMA AKAMWAMBIA LABDA URUDI NYUMBANI UKALALE KWA MKEO UTAWEZA KURUDI PEKE YAKO AKASEMA HAPANA KWAKUA ALIKUA ANAJISIKIA VIBAYA, YULE MAMA AKAWEKA VITU VYAKE SAWA AKAMRUDISHA KWA MKEWE
WAKAFIKA PALE AKAMWAMBIA MKWE BABA JAMES ANAJISIKIA VIBAYA SANA AKASEMA ANATAKA KWENDA KULALA ALIPOINGIA TU NDANI BABA JAMES AKAANZA KULALAMIKA KICHOMI JAMANI VICHOMI VINANIUMA WAKAMLAZA KITANDANI LAKINI ALIKUA ANALALAMIKA SANA KUHUSU VICHOMI ANAJIGEUZA TU KWENYE KITANDA
BAADAE WAKAMUONA ANASINZIA AKALALA, MARA KUMUANGALIA VIZURI AMEACHA KUHEMA NDIO KUSEMA LABDA KAZIMIA JAMANI KUTAFUTA WATU KUMKIMBIZA HOSPITAL KUSIKA MADAKTARI WAKAWAAMBIA AMESHAKUFA
BASI TARATIBU ZA MSIBA ZIKAWEKWA NYUMBANI KWA MKEWE, WATU WAKAANZA KULIA MSIBA, SASA KATIKA MSIBA VITUKO NDIO VIKAANZA MAANA KILA MTU ANALIA KIVYAKE MWENGINE BABA JAMES MWENGINE BABA ALLEN NDUGU WAKO WA PANDE MBILI TOFAUTI KILA MTU AKIMPOOZA NDUGU YAKE
MARA KATIKA HUHUO MSIBA KUKAWA NA DADA MMOJA KUMBE YEYE ANAKUAGA NA MAJINI JAPO MWENYEWE ANADAI HAYAJAWAHI KUMPANDA HIYO NDIO MARA YA KWANZA YAKAMPANDA NA KUMFWATA MKE WA YULE BABA NA KUMWAMBIA WEWE UMEMFANYA NINI MUME WAKO, LEO UTAONGEA UMEMFANYA NINI MUME WAKO BASI WATU NDIO KUSHANGAA TENA WAKUBWA WALIOKUWEPO NDIO KUMCHUKUA YULE DADA KUMPELEKA CHUMBANI KUMTULIZA HAYO MAJINI YAKE
ILA BAADA YA MUDA YANAMPANDA TENA NA KURUDIA VILEVILE KUONGEA NA YULE MKE MMHH NINONG'ONO IKAANZAA YA CHINI KWA CHINI HUKU MKE AKIWA TU ANALIA SANA AKIWA AMEVAA FUNGUO ZA CHUMBANI KWAO SHINGONI BILA KUTAKA MTU AINGIE HUKO
BASI MWILI UKASAFIRISHWA KWENDA TANGA KWENYE MAZIKO WOTE WAKAENDA BADO HAWAJARUDI KAMA YAPO MAPYA YALIYOJIRI NITAKUJA KUWAHADITHIA TENA.
*****END******
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz