Kero na maudhi katika ndoa ni zipi? - EDUSPORTSTZ

Latest

Kero na maudhi katika ndoa ni zipi?


Ni pale mke anapomsubiri mumewe kwa upendo arudi kutoka kazini ili aje kula mae pamoja ila hadi saa nane za usiku akawa mume bado hajafika nyumbani.
Ni pale mke anaamka asubuhi amemkasirikia mumewe bila kueleza sababu za kisirani chake kwa mumewe au wapi mumewe alipokosea.
Ni pale mume anaporudi usiku akiwa amelewa na kuanza kumporomoshea matusi mazito mkewe tena ya nguoni na kumuamuru afungue mlango mara moja bila kujali kuwa muda anaorudi mke na watoto wake wamelala.
Ni pale mke anapopotezea uwaminifu kwa mumewe na kuamua kutafuta ogomvi kwa lazima kwa kusubiri mume wake kaenda kuoga kisha anachukua simu na kuanza kumpekua na kuangalia mawasiliano yake ya kutwa nzima kuwa aliwasiliana na nani nani.
Ni pale mume anapokosa ustarabu na kuingia ndani na viatu au kuvutia sigara chumbani au sebuleni bila kujali harufu ya moshi wa sigara ni kero kwa wengine.
Ni pale mke anapokuwa na tabia ya kumjibu mume wake ovyo bila kujali watoto au majirani wanasikia au lah, mbaya zaidi bila kujali mume anapokeaje majibu yake ndani ya moyo.
Ni pale mume anapomfokea mkewe mbele ya wototo, majirani au hata ndugu bila kujali vile mkewe anavyojisikia moyoni.
Ni pale mke anapo anzisha safari yoyote bila kutoa taarifa kwa mumewe kuwa atakwenda mahala fulani.
Ni pale mume au mke anapotumia pesa vibaya bila kujali kuweka akiba kwaajili ya dharura na maisha yao ya baadae.
Ni pale mume au mke anapopigiwa simu na mchepuko wake muda ambao yupo nyumbani na mwenza wake na kuamua kutopokea simu, kitu ambacho kitampa wasiwasi mmoja kati yao kwa mwenza wake kutopokea simu.
Je, ni kero ipi inakukera zaidi kwa mke/mume wako katika ndoa au mahusiano yako?
"ITUNZE NDOA YAKO" whatsApp group 0717 442 212.
Au bonyeza link hapo chini ikupeleke moja kwa moja kwenye whatsApp inbox yangu
👇👇👇
Share
Like Page
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz