KAMA RAFIKI YAKO AKIKUFANYIA HIVI SIO SIFA JUA KAKUDHARAU MPAKA TONE LA MWISHO! - EDUSPORTSTZ

Latest

KAMA RAFIKI YAKO AKIKUFANYIA HIVI SIO SIFA JUA KAKUDHARAU MPAKA TONE LA MWISHO!

maishamahusiano Bilder - Instagram Bilder Über # maishamahusiano
Ni jambo la kawaida kwa mwanaume kumuona binti mzuri na kumtamani, akataka kuongea naye lakini akawa hana mawasilaino naye. Kama anajua hawezi kumuona tena na kuna namna anaweza kupata mawasiliano yake basi anaweza kuyaomba. Labda tuchukulie mfano ni dukani, ofisini, mtaani au sehemu yoyote, anaweza kuomba namba ya yule binti kwa mtu wake wa karibu, inaweza kuwa ni ndugu, rafiki, mteja au mfanyakazi mwenzake.
Narudia ni jambo la kawaida na kuna watu wanakutana kwa namna hiyo na wanakuja kuoana wanakua na furaha, wapo wengi na hupaswi kujisikia vibaya kama mwanaume akikutafuta na kukuambia namba yako nimepewa na flani au kuna mtu kanipa namba yako lakini kaniambia nisimtaje. Hilo sina shida nalo, lakini kama ikitokea rafiki yako, akakutana na mwanaume ambaye anajua moja kwa moja kuwa kaoa.
Narudia anajua kaoa, au hajaoa lakini anajua kuwa yule mwanaume ni kicheche ambaye ana mpenzi wake labda mchumba na wako siriasi, au hata hana lakini anajulikana na rafiki yako kua kuwa ni mtu wa kupita si mtu siriasi labda rafiki yako namba yako kwa mume wa mtu au mwanaume wa namna hiyo, lakini inawezekana kabla ya kutoa akakupigia simu na kukuambia “Kuna Kaka anataka hnamba yako!”
Achana na hivyo, rafiki yako anajua kuwa wewe umaolewa, au anajua una mchumba wako ambaye mko siriasi, anajua kuwa hata kama hamjawa wachumba lakini mko muda mrefu na unampenda au huyo mchumba wako anakupenda. Akagawa namba yako kwa mwanaume mwingine ambaye hata kama si mume wa mtu, iwe amekuambia kabla au baada lakini akagawa basi jua rafiki yako huyo kakudharau.
Narudia rafiki yako huyo atakua kakuona Malaya, anakuaona kama wewe ni rahisi unaweza kukubali kubali tu, lengo lake ni kukudhalilisha ili apate cha kusema kuwa yule anagawa gawa tu. Hivi kwa rafiki ambaye anakupenda atampaje mume wa mtu namba yako, anampa ili nini, angekua si mume wa mtu labda tungesema anampa ili uolewe anakupenda, ila anajua hutaolewa hivyo anatoa ili ugongwe na kuacha, labda kama na wewe mdangaji na unapenda!
Labda anajua jamaa ana pesa hivyo ni kama rafiki yako kakuona Malaya unapenda pesa. Tena mwingine anakumabia tumchune kabisa, nawewe bila kufikiria kichwa ndezi unakubali huku hata una mpenzi wako! Huyo mtu kakudhahrau kama ni mwanamke si yeye naye yuko kama wewe kama ni mwanaume huyo naye ni walewale aolewe yeye! Narudia si sifa rafiki yako kugawa namba yako kwa mwanaume ambaye anajua hawezi kuwa siriasi na wewe.
Lakini rafiki yako anajua una mume, anajua una mchumba, ushatambulishwa na una furaha, halafu anagawa namba yako kwa mwanaume mwingine, hapo kuna mawili, kwanza anakuona Malaya na pili anataka kukuharibia. Unatakiwa ujue kuwa kama kaweza kugawa namba yako, kama ukikubali kuongea na huyo mwanaume inamaana ni kama umekubali kufanya naye mapenzi lakini jua nilazima atakutangaza.
Hawezi kukufanyia siri, kila atakapokutana na yule mtu basi utasikia huyu si katembea na flani, hata kama hukutembea naye lakini si namba ilitolewa na wewe ukachekelea! Kuna wanawake wengi huharibu ndoa zao kijinga namna hii na wengina huharibu mahusiano yao kijinga namna hii. Hivyo kama rafiki yako akikuletea upuuzi huu, mwanaume kaoa au wewe uko kwenye ndoa muambie aache upumbavu na ampe yeye! Labda kama na wewe ni mdangaji hujajielewa bado, ila kama unajielewa na unajiheshimu utamuambie niondolee ulimbukeni wako hapa!
NISHAMALIZA KAMA UNA HII TABIA SOMA KIMYA KIMYA USI SHARE!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz