HEBU TUZUNGUMZIE MAUMIVU YA MAPENZI KIUFUPI - EDUSPORTSTZ

Latest

HEBU TUZUNGUMZIE MAUMIVU YA MAPENZI KIUFUPI

✍️Maumivu ya mapenzi yanaweza kukufanya ushindwe kuona umuhimu au umaana ya maisha Kwa maana
unaweza ukawa na mahusiano na mtu na umeweka malengo nae makubwa tu kumbe mwenzako hajawahi waza hilo na wala hana malengo na wewe anakutumia kwa manufaa yake tu.
✍️Ni muda sasa wa kuamka na kuanza maisha mapya bila kujali nani amekuumiza au kukuacha katika mazingira magumu.
✍️kama upo kwenye mahusiano na hamna ile hisia kama upo kwenye mahusiano ambayo wewe ndiyo muwajibikaji basi jua kuna walakini mahali.
Unampigia yeye tu yeye wala hawazi kukutafuta kutumia nguvu kuyaweka mahusiano yawe kama zamani au kusuluhisha ugomvi usioisha ni moja ya dalili mbaya.
✍️Tafakari kwa makini kabla hujachelewa.
Usiendelee kuwa na mtu ambaye hamaanishi na wala haonyeshi upendo kwako.
✍️kuwa na subira achana na mtu ambaye unamlilia kila siku. MUNGU atakupa mtu atakaye kuwa sababu ya kutabasamu na kuwa na amani moyoni pamoja na furaha ya kweli.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz