Wanaume njooni jandon
Unapata girlfriend/mchumba anakupenda na kukujali kwenye kila hali, anakupenda kupitiliza mpaka unajiona mwenye bahati kuliko wengine, dada wa Watu anajiachia kwako akijua wewe ndo utakuwa wake wa milele. Tatizo letu wanaume huwa linaanzia hapa, tunapopendwa kupitiliza huwa tunajisahau na kuanza kujiona kama miungu watu, tunaanza kuyachukulia mapenzi yake for granted, tunamuona anayetupenda kama vile amekosa mwingine wa kumpenda.
Hatujiulizi anafuatwa na wangapi na anawakatalia kulinda mapenzi yake kwetu, hatujiulizi ni wangapi wapo tayari kuwa naye ila wameikosa hiyo nafasi ukapatiwa wewe unayeichezea na kumuona aliyekupenda kama kapotea njia vile. Tumejisahau na kusahau kuwa naye ana moyo na anaweza kuamua lolote muda wowote, tumesahau kuwa naye ana maumivu kama ambavyo sie huumia.
Tusipopendwa vile tunavyotaka, tumesahau kuwa mapenzi ni pande mbili na si upande mmoja. Siku wakiamua kuondoka huwa ndio siku tunayokuja kutambua kuwa alikuwa na mapenzi ya kweli, ndio siku utakayojua kuwa kuna mapenzi ya kweli hapa duniani, ndo siku utakayoshtuka kumbe kumekucha na wewe bado una usingizi. Unapopendwa sana usichezee bahati uliyopewa, usitoe nafasi kwa mwingine akaja kuichukua ile furaha ambayo ulitakiwa kuipata wewe, usitoe nafasi kwa yule anayekupenda akalia juu yako, usije kujutia muda, mapenzi hayaji mara mbili, yakienda hayarudi, take it from me.
Post a Comment