UKIONA HIVI NI BORA UMUACHE AENDE - EDUSPORTSTZ

Latest

UKIONA HIVI NI BORA UMUACHE AENDE


MWACHE AENDE......
Ni kweli unampenda sana unamjari unamthamini sana, unajitahidi sana kumwonyesha upendo, ni kweli unataka kumwoa kabisa yaani. ebu fikria kwanza:-
Kila mkikosana ata kama kosa ni lake wewe ndo wakuomba msamaha wewe ndo wakulia lia mwenzio anaendelea na maisha yake utazani hakijatokea kitu.
Ukweli unaujua mwenyewe jinsi unavompenda sana kuliko ata unavompenda Mungu, na unafahamu jinsi anavokudharau anakuchukuliaga poa tu hata usipomtafta ww basi hamtawasiliana siku nzma yaani.
Kiugomvi kidogo tu anakwambia muachane ata kama kakukosea yeye duh acha hizo utavumilia mpaka lini
Ni kweli anakusaidia vitu vingi sana ni kweli ye ni mzuri sana but ni kweli huwezi kumpata kama yeye ila unaeza kumpata mzuri na bora kuliko yeye acha hizo jikubali mwache aende, we mwenyewe ukiwaza kwa kina unaona kabisa jinsi unavojipendekezaga kwake usikute unaonaga sms za wapenzi wake au hapokeagi simu akiwa na ww au ukitaka kushika simu yake anakua mkali simba hafiki yaani
Anakufanyia visa vingi sana kuna mda hadi unamfumania yaani but umekazana kuvumilia tu mmh ujinga huo ebu fikiria kama huo mda na hizo nguvu ungewekeza kwa BWANA YESU KRISTO si ungekua hodari kiroho na kimwili.
Mungu anakupenda sana, thamani yako kwa Mungu ni kubwa mnoo, nkwambie kitu wewe ni mzuri sana kizuri zaidi upo vizuri na Mungu sa unaogopa nini kama ni chaguo lako mwache aende kuna siku atachapwa na Mungu atarudi mwenyewe kirainiiiiii.
Usikubali kufanya mapenzi na mpenzi au mchumba wako ata mkiachana hautaumia sana, wahanga wengi ni wadada dah poleni sana jamani, Mwache aende utajikuta unapoteza bahati zako bure tu usikute kuna mkaka/mdada anakupenda hatari but anaogopa kukufata coz anajua una mchumba duh
Wewe ni mme bora wewe ni mke bora wewe ni mzuri hatari, uliumbwa na Mungu tena kwa mfano wake kabisa yani dah usilie futa machozi amka mwache aende maisha yaendelee, unajua nini
MARKO 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.....
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz