UFU BANDIA NI SHERIA... - EDUSPORTSTZ

Latest

UFU BANDIA NI SHERIA...

Happy together - young couple kissing. Lifestyle photo of young ...
UFU BANDIA NI SHERIA... lakini mtu anapokuwa anayo dhamira ya dhati yeye ndiye anatakiwa kuwa mwanzilishi wa kujenga maisha, Maisha utaratibu wake ni UTEKELEZAJI! Ukiona uko kwenye mahusiano ama ndoa na mtu ambaye anategea wewe ndo uwe mwanzilishi wa jambo lihusulo maisha JIONGEZE... Ni aibu kubwa kwa mwanaume kumtegea mkewe afanye MAISHA NAE kwa sababu eti yeye ni kichwa cha nyumba, Ndugu yangu hata kondoo anacho kichwa chake, Wewe ukijipa moyo kwa neno la MANABII KWAMBA MUME NI KICHWA CHA NYUMBA na hauwi kama maandiko yanavyotaka ujue UNAJIPA CHEO KISICHOKUHUSU😎
Kichwa gani hata hujui mkeo anavaa size gani ya skate? Kichwa gani mwaka unaisha wala hujawahi kubeba hata kilo moja ya nyama? Kichwa gani hujui hata ada ya mtoto wa kiuno chako? Kichwa gani wewe usiyejua kuwatunza wa nyumbani kwako? Nakuuliza wewe unayejitapa ni MUME na wala hujisumbui kumpenda mkeo, Ndugu yangu kama ulikuwa unatarajia kuoa kwa ajili ya MTEREMKO TARAJIA kula vyakula walivyonunua wanaume wenZio, Wewe si mvivu wa kuhudumia? Wacha ujidanganye kwa kuamini cheti cha NDOA huku mwenzio aliishakutoa moyoni na mwilini AMEKUFANYA KAMA PICHA ILIYOKO KWENYE FLAME🤣🤣
Man rudi kwenye misingi ya kiume wacha kupenda miteremko UNAJISHUSHIA HESHIMA KWA MWANAMKE WAKO🙋🏻‍♂
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz