Shughulikieni Tabia Zenu, Zikiwashinda Bora Muachane! - EDUSPORTSTZ

Latest

Shughulikieni Tabia Zenu, Zikiwashinda Bora Muachane!


MAPENZI ni uvumilivu. Watu mnakutana ukubwani, mnaanzisha uhusiano kila mmoja akiwa na hulka zake. Kila mtu amelelewa kwao, mnakutana na kutengeneza serikali yenu. Itakayokuwa na sheria moja, kusikilizana. Ukipata nafasi ya kuzungumza na wapendanao wengi kwa sasa, kila mmoja akakupa ushuhuda, utachoka. Simulizi nyingi ni za maumivu. Mwanamke anamlaumu mwanaume na mwanaume anamlaumu mwanamke. Kila mmoja anamuona mwenzake ni mkosaji. Mwanamke anajiona yupo sahihi katika mambo anayoyafanya, vivyo hivyo mwanaume anajiona yupo sahihi. Kinachofuata ni malumbano ya hoja. Mwanamke yupo moto, mwanaume ndiyo usipime! Mwanaume akikupa ushuhuda wake atakuambia amechoka. Amechoshwa na tabia za mwanamke. Amemkanya kwa muda mrefu lakini wapi, somo halimuingii. Ametumia kila aina ya njia kuhakikisha anamweka sawa mwenzi wake lakini inashindikana. Mwanamke vivyo hivyo. Atakuambia ameshughulikia tabia za mwenzi wake kwa kiwango cha juu lakini matunda yake ni hafi fu. Anaumia, mwenzi wake habadiliki kitabia. Mbaya zaidi anaendekeza mfumo dume, hataki kumsikiliza. Anaamini yeye ndiyo mwanaume basi yupo sahihi kwa kila jambo. Ukizungumza na wawili hao kwa nyakati tofauti, ukampa ushuhuda wa jinsi watu wengine wanavyoishi vizuri katika uhusiano, atakwambia kwake ni ndoto.

Mwanaume atakuambia anatamani mwanamke wa fulani angekuwa mpenzi wake kuliko mateso anayoyapata. Atauona uhusiano wa mwenzake ni bora kuliko wa kwake. Utasikia akitoa zile kauli za ‘natamani na mimi ningekuwa mpenzi wa fulani. Fulani anamjali mpenzi wake. Anaishi vizuri na mwenzake, hawana hata ugomvi wa mara kwa mara’. Mtu wa aina hiyo anaamini wenzake wana ahueni. Hataki kukubali kwamba hata hao anaowatamani nao wana matatizo yao. Pengine wanagombana, wanayamaliza kimyakimya bila kuwaeleza wengine. Yawezekana mambo yao ni mazito kuliko hata yao lakini wanayatatua bila watu kujua.

 ITIBUNI TABIA KWA NGUVU ZOTE
Kama nilivyotangulia kuwaambia awali, tabia ni jambo ambalo linajengeka kwa muda mrefu. Kumbadilisha mtu tabia inategemea na namna anayerekebishwa atalichukulia jambo hilo kwa mapokeo gani. Akiwa muungwana anaweza kupokea, asipokuwa anaweza kukataa. Anaweza kuona unamuonea. Anaweza kukuona una gubu. Ataihalalisha tabia yake mbaya kuwa tabia njema. Ataamini anachokifanya ni sahihi hata kama si sahihi.

 WENYE MALENGO HUWA WANASIKILIZANA
Hata iweje, wenye dhamira njema ya maisha huwa siku zote wanasikilizana. Wanabebwa na dhana pana ya pendo. Wanatanguliza uzalendo wa penzi lao. Penzi lao ndiyo kila kitu mengine  yote yatafuata baadaye. Wanagombana, ugomvi unakuwa mkubwa kwelikweli lakini wanapofi kiria dhana pana ya uzalendo wa penzi lao huwa wanarudi nyuma. Wanashuka, wanaelewana na maisha yanaendelea huku watu nje wakishindwa kubaini udhaifu wao. REKEBISHANENI MAPEMA Kipindi kizuri cha kurekebishana tabia ni wakati mkiwa katika hatua za awali. Uhusiano unapokuwa mchanga, ndiyo kipindi kizuri sana cha kurekebeshana tabia. Mwenzako ana tabia fulani, mueleze ili aweze kubadilika. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi, mkunje mpenzi wako kabla safari yenu haijafi ka mbali. Mueleze tabia fulani anayoifanya si ya kiungwana. Anapofanya jambo fulani si jema hivyo ajirekebishe ili muweze kwenda sawa.

KITU CHA KUZINGATIA
 Watu wengi sana huwa hawapendi kukosolewa. Unapomuambia mwenzako kuhusu tabia fulani aliyo nayo usitegemee majibu mazuri tu kutoka kwake. Yawezekana asipendezwe hivyo unashauriwa pia kutumia lugha rafi ki kufi kisha ujumbe. JIPIMENI Maisha ni uvumilivu, jipimeni kupitia uvumilivu wenu na namna ambavyo mnaweza kubadilishana tabia. Unayemueleza abadilike anakuelewa au anaamini kile anachoamini yeye ndiyo sahihi? Anachokueleza na wewe unakielewa? Ili muweze kufi kia muafaka ni hadi pale ambapo ataubeba udhaifu wa mwenzake. Kila mmoja akijiona yupo sahihi, mtaishi maisha ya kushindana kila siku. Mashindano kwenye uhusiano ni kirusi hatari sana. Mkiona mnashindwa kuchukuliana, kuelewana katika hatua za awali basi ni vyema kukatisha safari. Kama unamrekebisha mwenzako juu ya tabia fulani na mwenzako anaamini wewe ndiyo una tatizo unategemea nini? Mtabishana mpaka lini kama kila mmoja atasimamia msimamo wake? Kama unaona inashindikana kuelewana, ni bora muachane kwa heri na maisha yawe huru kwa kila mmoja wenu. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz