Mpe mpenzi wako kile wengine wasichowapa wapenzi wao! - EDUSPORTSTZ

Latest

Mpe mpenzi wako kile wengine wasichowapa wapenzi wao!


Niseme tu kwamba mapenzi ni idara ambayo ukiipatia, maisha yako yatakuwa ni ya furaha sana na utatamani kifo kisiwepo ili uishi milele lakini ukikosea kidogo tu unaweza kujikuta ni mtu wa kulia kila siku na wakati mwingine kujuta kwa nini Mungu alikuleta duniani.
Ndiyo maana huwa nasema, fanya maamuzi sahihi kwa kumchagua mtu sahihi ambaye moyo wako unaamini atakupata furaha uliyoitarajia.
Baada ya kumpata mtu huyo, tumia gharama yoyote kumshika vilivyo ili asikuponyoke. Hakikisha unamfanya akuone wewe ni wewe na bila wewe maisha yake hayajakamilika.
Hilo litawezekana kama tu utamjali kwa mambo muhimu ambayo nimekuwa nikiyaandika mara kwa mara kupitia safu hii. Sina sababu ya kuyarudia lakini leo nataka kugusia mambo matatu ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiyapotezea na mwishowe kujikuta wanayachukia mapenzi kwa sababu za kujitakia.
Ukijaribu kufuatilia kwa karibu utabaini kuwa, wapo wanawake ambao wamekuwa wakijitengenezea mazingira ya kusalitiwa bila kujua.
Wapo ambao hawajui nini wawape wapenzi wao ili kuwadatisha, wapo ambao wanajua wanachostahili kuwapa wapenzi wao ila kwa makusudi tu wanaamua kutowapa lakini baadaye wakitemwa wanaanza kulia.
Wanaume wanapenda vitu adimu kutoka kwa wapenzi wao, wanapenda vitu ambavyo wanahisi wenzao hawawezi kuvipata kutoka kwa wapenzi wao. Hivyo ndivyo unavyotakiwa kumpa mpenzi wako ili uweze kumshika.
Ninaposema hivyo simaanishi kwamba unatakiwa kumpa mpenzi wako mapenzi kinyume na maumbile, maana najua wapo ambao wameelekeza mawazo yao huko.
Chondechonde simaanishi hayo jamani.Tena naomba niseme kwamba wanaowapa wapenzi wao mapenzi kinyume na maumbile hawajipendi, wanayachukia maisha yao na wako tayari kwa lolote. Sikushauri kabisa ufanye hivyo kwani ni hatari kwa maisha yako.
Ninaposema umpe mpenzi wako kile ambacho wengine hawawapi wapenzi wao namaanisha mengi lakini haya yafuatayo ni ya msingi;
Utundu na ubunifu
Mapenzi ni utundu na ubunifu hasa unapokuwa kwenye uwanja wa sita kwa sita na mtu uliyetokea kumpenda sana. Onyesha utundu wako wote, tumia akili yako kubuni vitu ambavyo unaamini vitampagawisha mpenzi wako. Kwa kufanya hivyo unaweza kuwa wa kipekee kwake na ataamini amempata mtu sahihi.
Usimbanie
Katika hili naomba niseme kwamba mapenzi ni sawa na chakula. Mwanamke anayempenda mume wake anatakiwa kuhakikisha anampa chakula pale anaposikia njaa. Tena mwanamke huyo atampa chakula kwenye ‘hot pot’ kikiwa cha moto na mume atajisevia kiasi kinachomtosha.
Kwenye mapenzi nako ni hivyo hivyo. Mpenzi wako akihitaji kuwa na wewe faragha usitoe visingizio visivyo na msingi na muwapo faragha mpe uhuru wa kula apendavyo, kwa staili aitakayo ila hakikisha unamzuia asile ‘makoko’ kwani yana madhara kwake na kwako.
Kama utafikia hatua ya kumpa mpenzi wako mapenzi kwa ratiba au kumpa penzi katika mazingira ya kigoigoi, tambua siku zako za kuachwa zinahesabika.
Maneno matamu
Mumeo ni mtu wa kumpa maneno matamu kila wakati, maneno ambayo yatamfanya ajisikie kuwa pembeni yako kila wakati.Wapo wanawake ambao hawako makini katika hili na kujikuta ni watu wa kubwatuka ovyo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz