*MFURAHISHE MKEO KWA VITU RAHISI* - EDUSPORTSTZ

Latest

*MFURAHISHE MKEO KWA VITU RAHISI*

Kabla Hujalalamika Mpenzi Wako Ana Tabia Mbaya Jiulize Mara ya ...
......🍇🍇 _Mwanamke ni ulimwengu mpana sana ambao huathiriwa na hisia zake zaidi ya anavyoathiriwa na kitu kingine chochote._
......🍇🍇 _Mwanaume akifanikiwa kuumiliki moyo wake atakuwa amefanikiwa kukimiliki kitu kingine chochote._
......🍇🍇 _Wanandoa Maridhawa inakuletea ushauri na nasaha maridhawa za namna ya kuboresha uhusiano wako na mkeo kutokana na ukweli kwamba mwanamke anahitaji mtu anayempenda zaidi kuliko anayemuelewa._
*Yafuatayo ni mambo rahisi ambayo unaweza kuyafanya ili kuuteka moyo wake.*
*1. Zidisha ‘surprise’.*
......🍇🍇 _Leo mfanyie surprise kwa kitu fulani, siku nyingine kwa kitu kingine. Kwa mfano, unaweza kumfanyia surprise ya kwenda kula chakula cha usiku mahala fulani au ukaenda naye sehemu ambayo anaipenda na ambayo angetamani kwenda. Lakini panga safari hiyo kulingana na uwezo wako._
*2. Kuwa mwingi wa kumpa zawadi.*
.........🍇🍇 _Kadiri unavyolifanya suala hilo kuwa sehemu ya mazoea yako ndivyo unavyouteka moyo wake. Zawadi ni chochote, hata pipi ni zawadi._
*3. Usiache kumuuliza kuhusu hali ya ndugu na jamaa zake.*
......🍇🍇 _Fanya utaratibu wa kumpeleka kwao mara kwa mara ilia pate kufurahika nao._
*4. Kuwa kama baba, rafiki, kaka na uwe kila kitu kwake,*
.........🍇🍇 _Kwa sababu aliacha kila kitu kwao akaja kwako kwa ajili yako. Haipendezi ukamuacha usiku wa manane na kwenda kuangalia soka kwenye vibanda vya mpira wa miguu huku ukimuacha peke yake kitandani bila ulinzi wala usalama wowote._
*5. Usiwe mwingi wa kumfokea na kumpigia makelele,*
......🍇🍇 _kwa sababu silaha ya kwanza atakayoitumia dhidi yako ni kilio kisha atatamani kwenda kwao, hivyo nenda naye kwa upole na ulaini wa moyo na mwenendo wako._
*6. Usimwambie maneno yasiyokuwa mazuri.*
*7. Kuwa mwingi wa kusifu*
......🍇🍇 _Kila kitu anachokifanya nyumbani kama vile mapishi, upangiliaji wa nyumba, usafi na vitu vizuri anavyoviongeza kwenye muonekano maridhawa wa nyumba yenu. Jambo hilo litamhamasisha kutilia umuhimu masuala ya ndani._
*8. Mwambie maneno mazuri,*
........🍇🍇 _kwa sababu humlainisha anapoyasikia._
*BAADAENI IN SHAA ALLAH, NAKWENDA KUTAFUTA MUME WA PILI 🎀🎀BY QURTHUM*🎀🎀
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz