MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAISHA YAKO .. ukiyashika haya hutaweza kufeli katika safari yako: - EDUSPORTSTZ

Latest

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAISHA YAKO .. ukiyashika haya hutaweza kufeli katika safari yako:


1)Ukiona unaambatana na Marafiki ambao wanakupeleka Sehemu isiyompendeza Mungu, Usisubiri nakushangaa shangaa😳 chukua hatua 🤔 achana nao. Hata kama utaumia ni Bora ujiokoe mapema kabla ya kuangamia.(epuka ningelijua) Mpendwa ngeli haitangulii.
2)Ukiona unafanya jambo lolote hufanikiwi. Achana nalo kwa wakati huo. Kaa chini mwombe Mungu akupe njia nyingine . mpendwa maana unaweza kujikuta unachelewa kufika unakotakiwa kufika au ukajikuta unaziacha njia za Mungu ..
NDUGU YANGU
Kuliko mambo ya Duniani yakukoseshe ufalme wa mbinguni bora ukose yote hapa Duniani. Ndugu ,mali, mke,Mume,kazi nk. Nibora uvikose ili ufalme wa Mungu upate...
Soma mathayo👇
Matayo:18.6
bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Matayo:18.7
Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!
Matayo:18.8
Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.
Matayo:18.9
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.
Sema amen kama umenielewa
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz