KWENU WANA NDOA WOTE NA WALE MNAOTARAJIA KUINGIA KWENYE NDOA. - EDUSPORTSTZ

Latest

KWENU WANA NDOA WOTE NA WALE MNAOTARAJIA KUINGIA KWENYE NDOA.


Ndoa nyingi ni za kulala na kuamka, kulea watoto na kuzeeka pamoja hadi kifo kifike. Hii sio sahihi!
Ndoa lazima iwe ya kufurahisha na kimapenz.
1- Wanandoa wanabusu na kukumbatiana tu pale wanapopata habari njema.
2- Mume huweka chakula mdomoni mwa mkewe tu wakati anaumwa na hawezi kujilisha mwenyewe.
3- Ukiona mwanamme anamfungulia mkewe mlango wa gari, inawezekana huo mlango ni mbovu.
4- Kitu pekee kinachomfanya mwanamme wa kiafrika aguse shingo ya mkewe, ni pale anapolalamika homa. Hataigusa tena hadi homa ijayo.
5 Wakati pekee anaoweza kumbeba mke wake mikononi mwake ni wakati yuko katika " kushughurika".
6- Ukiona wamekaa nje usiku, usidhani wako romantic, wanasubiri harufu ya dawa ya kuulia wadudu itoweke.
7- Wake wengi huwanunulia waume zao zawadi wanapolazwa tu hospitalini.
8- Wakati pekee ambao wanakimbia pamoja ni wakati kuna hatari, na kila mmoja anakimbia kujiokoa.
9- Wakati pekee wanaooga pamoja ni pale ambapo kila mmoja anataka kuwahi kazini.
10- Wakati pekee wa mke kuangaliana kwa karibu na macho ya mumewe ni pale anapolalamika kuingiliwa na uchafu au mdudu machoni pake.
Waafrika wengi wanahisi, mwanamme akimpenda mke wake, Basi atakuwa amedhibitiwa na mkewe.
Tubadilike, na tujifunze kupendana katika ndoa zetu, ili kufurahia siku chache tulizo nazo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz