Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke Kwa Njia Ya Kirafiki - EDUSPORTSTZ

Latest

Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke Kwa Njia Ya Kirafiki

Beautiful gospel artiste confesses she struggles with 's@x' addiction
Wakati unapotongoza mwanamke huwa kuna vitu viwili; aidha unatongoza njia sawa ama unatongoza kwa kubahatisha.
Njia yeyote katika hizi mbili utakazozichukua, mwanamke atafahamu ya kuwa unajaribu kumpendeza na anajua unataka kutoka naye deti.
So matumaini yako hapo ni kuona ya kuwa mwanamke kama huyu anavutiwa na wewe bila kukukatiza tamaa.
Ok, unless huyu mwanamke anatafuta mchumba wa kudeti ama anatafuta mwanaume wa kujikeep naye buzy, kuna nafasi kuu akigundua ya kuwa unabahatisha kumtongoza, papo hapo atakuzima na kukuonyesha dalili za kuwa hakupendezwa na njia yako ya kujaribu kumuapproach.Akikukataa najua unaweza kuingiwa na misongo ya mawazo kutaka kujua kwa nini amekukataa. Unaweza kusumbuliwa na jambo hili kwa muda mrefu.
Lakini kama kawaida, kutongoza mwanamke huwa ni bahati nasibu, anaweza kukukubali ama kukukataa.
Well, leo nimeamua kuja na mbinu tofauti ya kutongoza mwanamke. Hii mbinu itamfanya mwanamke kuingiwa na maswali ya kujiuliza iwapo unamtongoza au la. Mbinu hii utamvutia mwanamke bila hata kumwambia neno "NAKUPENDA".
Zama nami
Jinsi ya kumtongoza mwanamke kiurafiki
1. Kuwa mwanaume bora
Katika dunia tunayoiishi sahizi kila mwanaume anatamani kuwa na mwanamke bora zaidi. Hivyo kutaka kuwa na mwanamke unayempenda lazima uwe bora kuliko wengine. Hii ni kuanzia tabia zako, vile unavyohusiana na wengine, miondoko yako, unadhifu wako nk. Kuwa mwanaume bora hakuna njia ya mkato. Lazima ufuate mkondo ambao wengi hawaufahamu.

UTAMU KITANDANI NI NINI?? 
(WAKUBWA TU 18+) : JIFUNZE MAMBO YA CHUMBANI TU 
2. Msifu vile inavyotakikana
Leo amekuwa tofauti kimwonekano?, ama leo amebadilisha hairstyle yake? Kama umependezwa na mwanamke mara nyingi utakuwa unanotice mabadiliko yeyote ambayo ameyafanya hivyo chukua nafasi yako kumsifia vile inavyotakikana.
Well, sasa kama unataka kumvutia ili umuingize katika mipaka ya kudeti unafaa utumie maneno ambayo hatoyasahau. Usitumie maneno ya kawaida. Jaribu kutumia maneno ambayo hayatasahaulika kwake na ambayo ni ya kibinafsi bila kuvuka mipaka. Mfano wa maneno kutumia:
Hilo shati ulilovaa ni zuri - linakufanya unapendeza zaidi ya tausi
Marashi mazuri - leo unanukia utamu ambao sijawahi kuunusa popote
Unaweza kumsifia mwanamke chochote kile ilimradi pindi utakapotamka tumia maneno ya kibinafsi. Hii itamfanya wakati mwingine atakapopaka marashi hayo atakumbuka maneno uliyoyasema. Kufanya hivi kunamvuta polepole na kukufanya wewe kuingia katika moyo wake.
Kutumia maneno kama "ngozi yako ni laini, hivi wakati wote unakuwa hivi?" ama "nimependa shati lako na vile jinsi limekubana katika mwili wako" hakufai. Kusifu kwa aina hii usithubutu kutumia kwa sasa kwani unaweza kuharibu mpango mzima.
3. Tafuta muda wa kuwa nyinyi peke yenu
Kumsuka mwanamke huwa ni bora zaidi wakati ambapo mko nyinyi wawili pekeenu. Kumsuka mwanamke mbele ya marafiki zako kutamfanya kukuona wewe hauko serious na mambo unayotamka hivyo ni bora wakati ambapo unachukua muda na kuwa na yeye pekeenu mnaongea.
Unaweza kumsuka kwa kutumia mizaha wakati ambapo mko na marafiki zenu. Lakini wakati ambapo mko nyinyi wawili, tumia maneno ambayo hatayasahau kiurahisi. Mfano unaweza kumwambia "wewe ndie unafanya siku yangu kuwa ya shangwe", "kukaa na wewe hapa najiskia niko huru" nk kutamfanya yeye kujiona spesho kwako.
Ujanja hapa ni kutumia maneno ambayo yatamfanya yeye kujiona spesho kuliko yeyote na amini usiamini mwanamke kama huyu atakuwa akifikiria mazungumzo yenu kwa muda mrefu.
4. Wanawake wanapenda ucheshi
Hivi wewe ni mcheshi? Kama jibu lako ni la basi usiendelee kusoma zaidi ya hapa mpaka uifahamu sanaa ya ucheshi.
Nadhani unafahamu ya kuwa njia ya kumvutia mwanamke lazima utumie lugha ya ucheshi mara kwa mara. Well, uzuri ni kuwa si lazima uwe na ustadi wa kuchekesha. Unaweza kuelezea matukio yako ya awali ambayo uliona yalikuchekesha. Kama mwanamke anaonyesha dalili za kukupenda, basi kila neno utakalolitoa kiutani atacheka.5. Msumbue mara kwa mara
Wakati mwingine kumsuka mwanamke kunaweza kuonekana kuwa ni kazi ngumu, lakini kitu muhimu ni yale mambo madogo madogo ambayo mnafanya. Kumsuka mwanamke si kutumia maneno matamu ya kimapenzi pekee bali pia zile tabia ambazo mnafanya wakati mnapokuwa mnaongea. Hii ni kuanzia kucheka hadi migusano yenu ya mara kwa mara.
Kama nyote wawili mnakuwa na furaha wakati mnapoongea, hio tayari ni njia moja rahisi ya kuashiria unamsuka. So kuivuka mipaka ya urafiki, unafaa kuivuta miguu yake mara kwa mara upande wako wakati ambapo ameongea kitu cha kuchekesha ama mnapocheka. [Soma: Jinsi ya kumpandisha nyege mwanamke bila kumfanya kitu]
6. Cheza na mazungumzo machafu
Hatua tano za awali ambazo tumezitaja ni za kujenga mazingira ambayo yanawaweka katika hali ya kuleta nafasi ya kusukana kiurafiki.
Wakati ambapo utachagua kuvuka hii hatua, nyote wawili mtakuwa mumeingia hatua ya kuanza kutongozana.
Wakati ambapo umepata nafasi ya faragha ama unapompigia simu, jifunze kuchanganya maneno yako. Kufikia sasa najua nyote wawili kuna tenshen flani ambayo itakuwa imejijenga kati yenu hivyo usiingiwe na wasiwasi kama utajaribu kuingiza maneno ambayo yamevuka mipaka. Mara moja au nyingine unaweza kuingiza maneno ya kimapenzi katika mazungumzo yenu. Hata kama atakwambia uachane na hayo maneno utakuwa umechukua hatua kubwa kuonyesha hisia zako kwake.
7. Leta hisia za mguso
Wakati unapomsuka mwanamke ni vizuri zaidi kama utatumia sanaa ya miguso. Mara kwa mara tafuta kisababu cha kumgusa. Aidha unaweza kumgusa viganja vyake, mikono, vipuli vyake nk. Na kila wakati ambapo utakuwa ukimgusa hakikisha unachukua muda wako kumgusa ili ahisi mkono wako kwa mwili wake. Kufanya hivi atakuwa akipenda kama utatumia mbinu ya kijanja.
8. Muombe mtoke out mara kwa mara
Mara moja wakati wa maongezi yenu unaweza kumuomba umtoe mwende mkahawani ama kumpeleka katika sinema siku ya pili. Wakati mzuri wa kumwambia haya ni wakati ambapo mmemaliza maongezi yenu ama wakati mnapokuwa mnatext. Kumuuliza hivi si lazima uonekane uko serious na vile unavyosema. Kumaliza maongezi yenu kwa ghafla kutamwacha mwanamke kama huyu kujiuliza maswali iwapo ulikuwa uko serious wakati wa kumwambia wataka mtoke out ama ilikuwa tu mizaha.
Siku ya pili mkumbushe tena kuhusu deti yenu lakini usionyeshe kama uko serious. Kama atacheka pia wewe cheka halafu ujeuze mada. Labda atakuwa hajui kama uko serious ama ni mzaha ama bado hajapenda wazo la kwako kutoka deti na wewe.
Kama atakubaliana na mwitikio wako, kila la heri kwako. Iwapo atakataa basi anza tena mikakati yako ya kumridhisha mpaka aingiliane.
NB: Mara nyingi kama utafuata hatua za awali vizuri, mwanamke kama huyu hawezi kukataa mwitikio wako.
9. Zile simu za usiku wa kiza
Usiku huwa na mbinu ya kufurahisha kuamsha hisia zetu za mapenzi.
Marafiki wowote wawili ambao wanaongea kwa muda mrefu nyakati hizi za kiza mara nyingi hufikia hatua hii. Kama wataka kujua jinsi ya kutongoza mwanamke ili akupende chukua nafasi ya kumpigia simu ama kumtext nyakati kama hizi. Hakikisha ya kuwa unamrushia maneno ya kumtongoza.
Wakati huu wa usiku ambao umetulia ukiwa unaendelea na maongezi yenu ni rahisi sana kwenu kuivuka mipaka ya kuwa marafiki na kuanza kuonyeshana hisia zenu za mapenzi.
10. Mwonyeshe kuwa wewe unaweza kuwa mwenza mzuri wa kudeti
Ok kufikia sasa utakuwa umeshamwonyesha hisia zako zote, umemvutia na kujenga kemia za kimapenzi kati yenu, lakini utakuwa bado hujafunga mchezo. Atakuwa labda amependezwa na maongezi yenu na pia kukupenda kisiri, lakini kumfanya mwanamke akuone wewe kama una nafasi nzuri ya kuwa mwenza wake lazima uonyeshe dalili.
Wakati wa mazungumzo yenu, unaweza kutoa fununu za kuwa unatafuta girlfiriend ama unatafuta mwanamke wa kutoka naye out. Kama yuko single ama katika mahusiano mabaya, kitu kitakachokuja akilini mwake ni wewe na yeye katika hali kama hio, mwanzo itakuwa bora kama utachukua nafasi ya kuongea haya yote nyakati hizi za kiza.
Pindi utakapojua kutumia mbinu hii ya kutongoza mwanamke kiurafiki, kazi yako itakuwa imerahisishwa ya kutongoza kwani utakuwa ukitumia mbinu ambayo si ya kubahatisha.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz