JINSI SMS INAVYOWEZA KUFANYA MWANAMKE AKUTAMANI - EDUSPORTSTZ

Latest

JINSI SMS INAVYOWEZA KUFANYA MWANAMKE AKUTAMANI


Unaweza dhania kuwa kutuma ujumbe mfupi kwa mwanamke ili umsisimue haifai. Lakini kusema kwa hakika, inawezekana kumtumia mwanamke SMS ambayo inaweza kumsisimua na pia kupata atenshen kutoka kwake. Hii inaweza kufanya kazi vizuri iwapo umeingiwa na kibaridi cha kuongea na mwanamke moja kwa moja.

Kabla ujumbe ufupi kuvumbuliwa, wanaume walikuwa wakifuata mbinu nyingine kuonyesha kuwa wamevutiwa na wanawake waliowapenda. Walikuwa wakituma barua, kuambia rafiki wa rafiki zao ama kuwafuata na kuwapigia mbinja majumbani mwao. Lakini kwa bahati nzuri, hivi sasa kuna SMS, ambazo zina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi hapo kwa hapo kwa mwanamke ili kurahisisha kazi yako ya kutongoza.

Kabla hujaanza kumvutia mwanamke, ni lazima kwanza umfanye akutambue kwa njia chanya kwanza. Mwanzo haupaswi kutumia SMS kumsisimua mwanamke mpaka ile siku ambayo utapata kumsoma na kumjua zaidi. Lazima ujipatie muda ili ujenge connection kati ya nyinyi wawili ili iweze kufanya kazi. Kufanya hivi kutatoa picha ambayo itajijenga katika akili yake wakati munatumiana jumbe za kimapenzi. Kama ulimpendeza sana ile mara ya kwanza alipokupatia namba yake ya simu, basi itakuwa rahisi kwa mpangilio wako uende sambamba kama vile unavyotarajia.

Pindi utakapoingia katika level nyingine ya kuliwazika na huyu mwanamke ambaye unamrushia mistari, mwonyeshe vile ambavyo umependezwa na yeye kwa kumsifu. Hakikisha kuwa unakuwa mpole katika SMS zako pia. Kama yuko darasani au kazini, usimtumie jumbe mpaka ule wakati ambao yuko huru na makini wa kujibu texts zako.

Kama hujui ni wakati gani atakuwa yuko free, unaweza kujaribu kumtext wakati uo huo ambapo amekupatia namba yake ya simu (hakikisha una makinika kama utaamua kumtumia jumbe wakati uo huo ili usionekane kuwa una uhitaji mwingi). Vizuri zaidi wakati unapomtumia huo ujumbe unapaswa umsifie kwa jambo ambalo umeliona wakati ambapo ulikuwa naye awali. Mfano unaweza kumsifia kitu ambacho ulikiona kama vile nguo nzuri, tabasamu lake, macho, mawazo yake nk. Jaribu kuhepa kugusia umbo lake wakati huo.

Kama umekuwa mkitumiana jumbe kwa muda sasa na mumetoka deti mara moja au mbili, unaweza kuanza kuingiza na kugusia maswala ya mapenzi katika SMS zenu ili kuanza kupasha misuli kwa mambo ambayo unamwandalia usoni.

Kutokana na mistari ambayo umekuwa ukiisoma kwa mitandao ama kuiskia kwa marafiki zako, unaweza kuanza kumtext mwanamke huyu mara moja moja huku ukitulia ukiskilizia kama atakujibu kwa kukubaliana nawe ama kukupinga. Ukiona kama kila ujumbe anaoujibu anajibu kwa njia chanya, basi ni wakati wa kwako usichelewe tena bali uhakikishe ya kuwa unatumia mbinu ambayo utaingiza mawazo yako kwa akili yake na hatokusahau milele – huwezi jua, labda meseji utakayomtumia baadaye itakuwa ndio meseji ya kumfanya ageuke kuwa mpenzi wako.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz