JE , MWANAUME KUKOSA PESA KUNAFANYA UNYANYASIKE KWENYE MAHUSIANO?: - EDUSPORTSTZ

Latest

JE , MWANAUME KUKOSA PESA KUNAFANYA UNYANYASIKE KWENYE MAHUSIANO?:


Kuna baadhi ya wanaume wananyanyasika kwenye mahusiano, Upendo wanao mwingi ila pesa inafanya washindwe kujivunia upendo walio nao. Ni dhairi kizazi cha sasa wanawake wengi wanapenda pesa kwenye mahusiano, kabla ya kuangalia upendo.
👉Najua kuna vijana wanaupendo wa dhati, wanapenda kweli lakin ukosefu wa pesa unafanya upendo wao kutokua na faida yoyote mbele ya mwanamke. Kila mwanamke unaejaribu kumtongoza anaangalia ukubwa wa mfuko wako. Nikweli kabisa huna chochote lakin hakuna mwanamke anaekuelewa.
👉Unapambana mchana na Usiku, kazi ngumu za kukoroga zege, kuchimba mitaro au vyoo, kulima vibarua, kuosha magari, ujenzi, gereji n.k ni pesa ndogo unalipwa kwa kutwa. Unafikiria juu ya maisha yako, Utakula nn, utavaa nn, unahitajika kodi ya nyumba. Moyo pia unahitaji kupenda lakin umpendae hakuthamin tena anaona unampotezea muda.
👉Upendo wako unakua si chochote bila pesa. Unakaa mahali unawaza kwann maisha yangu yamekuwa hivi, pengine hukupenda, pengine ulitaman kusoma ila uwezo wa wazazi na familia uliishia hapo ulipo. Pengi ulivyobaki yatima ndipo maisha yako yakapoteza muelekeo.
👉Mwanamke anakufanya unajuta kuzaliwa, unajiona huna thamani duniani, Unalia sana lakin Chozi la mwanaume halina thamani chini ya jua. Upendo wako unakunyanyasa, Unatamani kufa. Unajiuliza Why me!
👉Nakwambia Hivi Inua kichwa juu sema na mungu wako, Piga moyo konde, Endelea kupambana. Hakuna aliezaliwa ili ateseke, Nikwasababu bado hujampata mwanamke sahihi wa moyo wako na wakati ukifika maisha yako yatanyooka tuu.
👉Bibilia Inasema Kwenye Kila mafanikio ya mwanaume, Kuna mkono wa mwanamke nyuma. Amin nakuambia yote unayoyapitia, yana mwisho. Unadharauliwa na mwanamke mpumbavu lakin utaheshimiwa na mwanamke mwenye akili, Huo Huo Upendo wako utakupa mwanamke wa maisha yako Kwasababu Mafanikio yako yapo mikononi mwa Mwanamke.
J4REAL

Image may contain: 1 person, standing and indoor
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz