Upweke, kwa hakika, huzaa migogoro isiyokwisha inayowafanya wanaume [ambao kimsingi ndio wasababishi wa upweke huo] washindwe kuwaelewa wanawake. Kwa mtazamo wao, ni vigumu kumridhisha mwanamke. Wengine wanaenda mbali na kufikiri , ‘mwanamke ni kiumbe mgumu kueleweka’ kwa sababu, ‘hata ufanye nini…hata umpe nini hawezi kuridhika’.
Lakini wanachosahau wanaume wenye mawazo haya ni kuwa mwanamke kwa asili yake anayo mahitaji ya msingi ambayo yanapopuuzwa, chochote kinachofanyika kama mbadala wa mahitaji hayo hakiwezi kuwa na maana yoyote. Usipoweza kujua mahitaji yake halisi, unaweza kumpa chochote kile unachodhani anakihitaji na bado mambo yasiende kama unavyotamani iwe.
Kusema hivyo, haimaanishi sielewi kuwa wapo wanawake wengi wanaopenda kujipatia fedha kwa wanaume. Hawa ni wanawake wanaofanya biashara ya mahusiano. Kwao, hakuna sababu yoyote ya kuwa na uhusiano imara na wenzi wao isipokuwa mpangilio wa kujipatia vitu na fedha.
Hatuzungumzii uhusiano huo wa kibiashara kati ya mwanamume na mwanamke bali uhusiano wa dhati unaojengwa katika misingi ya upendo, uaminifu, kuelewana na ahadi ya kuwa pamoja katika dhiki na raha.
Hebu na tutazame mahitaji makubwa ya kihisia aliyonayo mwanamke mwenye upendo wa dhati kwa mwenza wake.
Kupendwa kwa vitendo
Tulishaona kuwa hadhi ya mwanaume inategemea kwa kiasi kikubwa namna anavyoheshimiwa. Kwa mwanamke hali ni tofauti. Hadhi yake inategemea namna anavyopendwa na mwenzi wake.
Upendo kwa mwanamke unaeleweka anapoambiwa bila kuchoka neno nakupenda.
Mwanamke anapenda zaidi anachokisia kuliko anachokiona,nadhani hata biblia inathibitisha hili.mwanamke anahitaji kubembelezwa kila wakati
Kumtia moyo anavokata tamaa
Wanawake kwa asilimia kubwa ni warahisi kukata tamaa na wana mioyo miepesi,hivo ww kama mwanaume unajuku la kuhakikisha unakua bega kwa bega kumtia moyo mke wako.
No comments:
Post a Comment