JE MPENZI WAKO YUKO MBALI NA WEWE?? FANYA HIVI KUDUMISHA MAPENZI YENU - EDUSPORTSTZ

Latest

JE MPENZI WAKO YUKO MBALI NA WEWE?? FANYA HIVI KUDUMISHA MAPENZI YENUSiku zote mapenzi huyapa maisha thamani lakini wapo ambao hujikuta kwa namna moja ama nyingine wanatengana na wapenzi wao kwa sababu tu ya mihangaiko ya kila siku yakujitafutia ridhiki, masomo na wakati mwingine utengano huwa ni matokeo ya wapendanao kuishi sehumu tofauti hii huwakumba sana wanafunzi wa vyuo na shule za bwen

Umbali hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa.i.Hata hivyo, mapenzi ya mbali huna ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa muhanga kwa kuamia anakoishi ama kufanyia kazi la azizi wake. Hata hivyo, mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya haya:-
Mawasiliano ya mara kwa mara
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.

Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliyembali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe!

Heshimu hisia zako
Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi.

Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.

Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake, lakini sio ule wakubomoa! Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonyeshe unampenda.

Umbali si kigezo cha kunyimana
Mpe mwandani wako raha kamili kama ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila shaka unajiuliza inawezekanaje? Hili linawezekana kwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano. Mfano kama nyote mna simu jiandaye vyakutosha nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu ambayo utakuwa huru kuongea ama kufanya chochote kitakachokufanya uhisi raha isiyo na kifani na kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro bila kutarajia.

Bila shaka kila mtu anamfahamu vema mpenzi wake na hasa nini hupenda kufanyiwa ili aweze kufika safari yake na kama ndivyo basi hakikisha unafanya mambo yote ambayo ukimfanyia mwenzi wako pindi mnapokuwa kwenye mambo furani hupagawa.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz