Hatua 3 Za Kufuata Unapomtongoza Mwanamke - EDUSPORTSTZ

Latest

Hatua 3 Za Kufuata Unapomtongoza Mwanamke


Kama unataka kumpata mwanamke unayemzimia bila tatizo lolote basi hakikisha unafuata kila kitu ambacho utasoma sahizi. Hii mbinu imeibwa kutoka kwa kitabu cha Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani - ambacho nakipendekeza kwa yeyote yule ambaye yuko tayari kutumia maujanja ya mazungumzo kumnasa mwanamke yeyote.


Inaenda hivi...

Hatua #1: Angalia ishara.  Ufunguo wa kutongoza ni kuzijua na kuzivumbua ishara fiche kwa yale anayofanya na kutenda. Makinika na stori ambazo anaeleza, mambo ambayo anapenda kuongea na kila kitu ambacho kinaamsha hisia zake. Kumbuka hapa unamakinika na mwanamke na wala si wewe. Usijaribu kutoa maoni  yeyote bila kufikiria madhara yake. Unataka kumtongoza - na hautaki maoni yako yaonekane kama kipingamizi.

Hatua #2: Cheza na hisia zake.  Hapa jambo muhimu la kufahamu ni kuwa - kwa kuchagua mambo yafaayo kumwambia mwanamke, unaweza kubadilisha hisia zake hadi vile unavyotaka wewe. Huu uwezo wa 'kubadilisha' hisia za mwanamke ni jambo MUHIMU zaidi ya yote ikija katika maswala ya kumtongoza mwanamke.

Ingiza hisia nyingi iwezekanavyo katika mazungumzo yako kwake. Jibu stori zake na hisia zifaazo na utakuwa umejitenga mbali na wanaume wa kawaida ambao wanamuapproach.

Hatua #3: Mpe uhakikisho. Kila mwanamke (hata kama ni mrembo kiasi gani ama 'amekamilika' mbele ya macho yako) huwa wanakutojiamini ndani yao ambako kunahitajika kupewa uhakikisho kwa njia moja au nyingine. Hivyo hivyo, jambo muhimu la kuzingatia wakati unampa uhakikisho ni pale ambapo utakuwa mkweli wakati ambapo unampa huo uhakikisho.

Kumwambia kuwa ana macho mazuri hakutasaidia - hii ni kwa sababu maneno kama haya yashatumika mara kwa mara, na kila mwanaume anatumia maneno yayo hayo kama anataka kuingia ndani ya chupi ya mwanamke. Kumpongeza na kumpa uhakikisho kwa jambo ambalo hajiamini nalo kutamfanya akuthamini na kukuweka karibu na yeye zaidi. Na kama umefuata hatua hizi mbili za kwanza vizuri basi hautakosa kupata jambo ambalo litampendeza.

Huu uwezo wa kumtongoza mwanamke kwa kutumia maongezi ni advantage ya kikweli ambayo mwanaume anapaswa kuwa nayo. Ni jambo ambalo ni bora kuwa nalo kama unataka kuwa na nafasi nzuri kwa mwanamke yeyote.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz