GHARAMA YA KUWA MUME NI UPENDO💘 GHARAMA YA KUWA MKE NI UTII💑 - EDUSPORTSTZ

Latest

GHARAMA YA KUWA MUME NI UPENDO💘 GHARAMA YA KUWA MKE NI UTII💑


Wengi wanafurahia kuwa na wenza kwa sababu ya jinsia huku wakitamani kudumisha UHUSIANO/NDOA yao kupitia MTOTO/WATOTO💯
Ni rahisi sana kuwa BABA kuliko kuwa MUME.
Vile vile ni rahisi kuwa MAMA kuliko kuwa MKE kwani Mama na BABA wanatokana na kujamiiana, Ila Mke au Mume wanatokana na MAPOKEO YA NAFSI kwamba Mtu Mme atampenda Mtu Mke na kwa pamoja watakuwa na sababu ya kuwa wamoja📌
Heshima ya BABA ni kwa kuitunza familia yake na kuwapa FURAHA NA AMANI lakini kwa upande wa MAMA ili heshima yake iandikwe ni pamoja na KUMTII Mume wake bila kusahau jukumu lake kuwapa elimu elekezi watoto wake.
Hivyo kuna haja ya Watu kutofautisha nafasi ya MUME/MKE na nafasi ya BABA/MAMA kwani ni majukumu mawili tofauti japo yanatokana na maana moja MAPENZI😅😅
Sio kila MAMA au BABA anaweza kuwa suruhisho la hitaji la NDOA
Maana ili Mtu Mke ama Mtu Mme awe suruhisho la NDOA anawajibika kujua kwamba MTOTO analeta heshima ya kuitwa MZAZI na jukumu la NDOA halifungamani na wewe kuwa mzazi kwani kwenye NDOA ni eneo salama kwa ajili ya PACKAGE OF LOVE 🎁 peke yake.
Mtoto ama watoto hawapashwi kusababisha FURAHA NA AMANI kwenye NDOA yenu kwani hupatikana baada ya NDOA KUFUNGWA na hata kwa wale mnaozaa kabla ya kufunga NDOA Mtoto abakie kuwa zao PENDO lenu.
Mnaofungamanisha MTOTO/WATOTO na jukumu lililowaunganisha MAHUSIANO/NDOA mnakosea sana, Kwani Mtoto hawezi kuwa sababu ya kuzuia Maamuzi yatokanayo na MAHUSIANO AMA NDOA kwani yeye ni BAADA YA HAYO kwa vyovyote hana mamlaka na UTASHI WA MZAZI WAKE💯
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz