EBU TUAZIMANE MACHO HAPA NIKWAMBIE UKWELI BILA KUPEPESA MACHO YANGU - EDUSPORTSTZ

Latest

EBU TUAZIMANE MACHO HAPA NIKWAMBIE UKWELI BILA KUPEPESA MACHO YANGU


Kuna watu watataka kukurudia si kwasababu wamekukumbuka au bado wanakupenda, hapana wengine ni kwa kuwa tu wanakuona unaweza kuwa na furaha bila wao. Kwa muda mrefu kwa kuwa ulikua mwema kwao, kwa kuwa ulikua ukifanya kila kitu wanachotaka wao basi wanakuwa wakiamini kuwa huwezi kuishi bila wao. .
.
Mkishaachana wakakuona kuwa huwahitaji tena, unafuraha zaidi bila wao huku wao maisha yakiwapiga basi hujifanya kurudi.
.
Kuwa makini sana na mtu ambaye alikuumiza anapotaka kurudi tena katika maisha yako, kabla ya kukubali ebu jiulize ni kitu gani kimebadilika, je ni wewe umebadilika au ni wao wamebadilika? .
.
Wengi wanaotaka kurudi ni vidudu mtu ambao wanaumia mambo yao hayaendi wakati wewe ndiyo kwanza unaanza kunawiri! Kama mtu alikuacha na anataka kukurudia basi angalia sana sababu! .
.
Usisikilize sana maneno yake bali chunguza na kujua sababu inayo mrudisha JE NIFURAHA YAKE AU YAKO ? Usije kua ngazi ya kufanikisha tabasamu yake kisha akakudamp tena kwa dharau na kejeli .
SHARE NA WENGINE WAPATE KUJIFUNZA
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz