zangu, kama umewahi kuongea na mimi nimekuambia mambo mawili, kwanza usibebe mimba yake, pili usifanye maamuzi makubwa bila kunipigia. Simu yangu inakua bize sana, lakini najitahidi kupokea, naweza kukuambia subiri hata mara mbili lakini una haraka gani? Wakati naongea na wewe kuna kitu nilikiona, kuna ukweli niliupata kwako ndiyo maana nikakuambia usibebe mimba yake!
Nilijua kuwa huyo jamaa kuna namna anakudanganya, nilijua kuwa ukifuata ushauri wangu atarudi na kujifanya kabadilika, nilijua kuwa kwakua mnapenda kudanganywa basi utakubaliana na yeye. Ndiyo maana nilikuambvia unitafute mimi ili nikuonyeshe uongo wake. Kuna huu ujinga ambao mnasema “Kaka iddi nilidhani nitakusumbua!” nani alikuambia kuwa nasumbuka?
Kuna wengine mnasema “Kaka Iddi tatizo lako mkali!” Huyo wa kwako si mpole mbona kakutelekeza. Inauma sana unakuta binti wa miaka 22 kapewa mimba na mzee wa miaka 50 kisa tu alidanganywa nataolewa, wakati hapo ulishaongea naye na kumuambia huyo mtu anakupotezea muda wako! Inatia hasira pale ambapo mtu umetoka kuongea naye anaenda kumtambulisha mwanaume kwao wakati ushamuambia huyo mtu kwa dalili zake ni mume wa mtu!
Halafu mnajua mimi ni mpare, tumeongea leo nimekuambia kuwa huyo mtu ni muongo tapeli, eti baada ya miezi mitatu unaniambia uimempa milioni 20 kisa kajitambulishwa kwenu na katoa mahari! Najua mna hamu sana ya kuolewa, najua wakati mwingine naongea kwa ukeli, najua ni wapweke sana, najua kuwa mna mawazo sana, lakini hembu kama ushanunua kitabu changu nitumie, mbona mimi nipo tayari kuwa mnyama kazi, nitumie kabla ya kuharibu maisha yako!
IDD MAKENGO
No comments:
Post a Comment