WANAWAKEEE!! LEO NGOJA NIKWAMBIE USILOLIJUA KUHUSU WANAUME - EDUSPORTSTZ

Latest

WANAWAKEEE!! LEO NGOJA NIKWAMBIE USILOLIJUA KUHUSU WANAUME

Mwanaume anayeteseka katika ndoa yake, mara nyingi hasemi, hata akitaka kuchepuka, ni nadara sana mwanaume ambayekalaliwa na mke wake, mke wake anamsumbua, mke wake ni kichomi, mke wake anachepuka na ana wanawaume wengine kusema. Kwanza wanaume tunaona aibu, na kwetu kusema eti nachepuka kwakua mke wangu naye anachepuka, nachepuka kwakua mke wanguana matatizo haya na haya, mke wangu ananinyanyasa kwetu hiyo ni ngumu sana , si uanaume.
Najua ushaanza kuwaza “Mbona mimi yule Baba aliniambia kuwa mke wake alimsaliti, mke wake ana wanaume, mke wake ni mtu wa matumizi, mke wake anamnyanyasa… mbona alisema hata yule mtoto wao wa mwisho hana uhakika kama ni wake?” Dada yangu wala usishangae, wewe umetongozwa na Baharia, ukiona mwanaume anatongoza kwa kumkashifu mke wake basi jua kuwa huyo anajua madhaifu ya wanawake, ana uzoefu wa kutongoza, anajua kuwa njia rahisi ya kumpata binti ukiwa umeoa ni kumponda mke wako.
Yaani wanawake wanapenda sana kusikia mwanamke mwenzao akipondwa. Ukimuambia mwanamke “Mke wangu angekua na akili kama wewe tungekua mbali!” Basi kabinti ka watu kanasikia raha mpaka kufika kileleni kabisa hata kabla ya kuguswa bila kujua kuwa mwanaume kakuona fala hata akili anajua huna na kweli ukimkubalia kwasababu kakuambia hivyo basi jua kuwa una akili za kuvukia barabara tu! Hii sauti naona haitoishi niseme tu kuwa kama unamkubali mkubali kwakua na wewe una shida zako!
Lakini unakutana na mwanaume anakuambia “Mimi mke wangu ni kukaa tu nyumbani, nimemfungulia miradi mingi lakini hata hajishughulishi anaiacha inakufa!” Dada yangu jua huyo mwanaume ni Malaya na mke wake hafanyi kazi si kwakua hataki bali jamaa kamkataza kwani jamaa anajua kuwa kwa tabia zake mke wake angekua anafanya kazi basi angemuacha! Kwa maana hiyo wakati unajishaua kuwa anakusifia una akili basi jua kuwa akili anazozungumzia ulizo nazo ni za kuvukia barabara!
Ndiyo maana badala ya kufanya maisha, unaanza kuwaza kufanya maisha na mume wa mtu, unafanya Biashara na mume wa mtu, unamshauri kujenga, labda amekuona una nyota ya Biashara anakushirikisha kwenye mambo yake, lakini hamuachi mke wake na wewe badala ya kufanya mambo ya maana unafanya kazi ya kumsaidia yeye kufanikiwa tu yeye na mke wake. Sikuhukumu kwa kutembea na mume wa mtu kwani kila mtu ana dhambi zake, lakini nakushangaa unavyodhani anakupenda kuliko mke wake wakati hata hataki kumuacha!
IDD MAKENGO
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz