USIUSIFU MVUTO WA MARAFIKI ZAKO MBELE YA MUMEO/ MKEO - EDUSPORTSTZ

Latest

USIUSIFU MVUTO WA MARAFIKI ZAKO MBELE YA MUMEO/ MKEO


Miongoni mwa sifa muhimu za mwanamke mwerevu na mahiri ni kutousifu mvuto wa wanawake wengine mbele ya mume wake.
Licha ya kwamba jambo hili halikubaliki, lakini pia inamuepusha na majaribu mbalimbali. Vilevile, miongoni mwa sifa za mwanamke mwerevu ni kutousifu mvuto wa mumewe mbele ya marafiki zake.
Jitahidi sana kuifanya akili ya mumeo isishughulishwe na mawazo ya kukulinganisha wewe na wanawake unaowasifu mbele yake.
Kuwa mwangalifu usimuweke mumeo katika majaribu.
Kadhalika, miongoni mwa sifa thabiti za mume mwema ni kutousifu uzuri na mvuto wa mkewe mbele ya marafiki zake ili kutosababisha majaribu.
Jitahidi kwa kadiri uwezavyo kumfanya mkeo kuwa mtu mahususi na maalum kwako, usimfanye kuwa kama biashara inayotangazwa ili inunuliwe. Kufanya hivyo ni kuwaweka marafiki zako katika kisima cha majaribu.
Aidha, jitahidi mno kutoyasifu maumbile na mvuto wa marafiki zako mbele ya mkeo, kwa maana hilo litazalisha ushawishi katika fikra na kuishughulisha akili ya mkeo.
Like
Share
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz