*USHAURI KWA BOYS WOTE* - EDUSPORTSTZ

Latest

*USHAURI KWA BOYS WOTE*


*KUWENI WAZI KWA MABINTI*
Kama una date na binti wa umri wa kuanzia miaka 23 kuendelea na hauna mpango wa kumuoa fanya jambo la kiungwanana kumuambia ukweli.
Sikuambii umuambie kuwa humtaki na hutaki kuoa bali muambie kuwa wewe si muoaji na unaona kama utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza.
Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano
Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. Kwa Mwanamke, Age is not just a Number Age is Everything.
Wakati ukimuacha wewe utatafuta binti mdogo zadi yake, yeye atalazimika kutafuta Kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo, sote, Wanaume na Wanawake huangalia Umri katika Mahusiano.
Ukimchezea na kumuacha akiwa katika Umri wa Miaka 30, ina maana atafute kijana mwenye Umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado yuko Single. Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kuwa hawezi kupata, hapana, bali nasema utampa Wakati Mgumu na Uhuru wa Kuchagua.
Kuna Umri ambao Mabinti wengi huamua Kuolewa tu, si kwasababu ya Mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri Mtu Sahihi watapishana na Kalenda.
Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu Miaka Mitano halafu unamuambia Wewe si Type yangu Fanya jambo la Kiungwana na Malizaneni Mapema. Lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha. Mlazimishe asikie na Usimtumie na Kumuumiza kwa kuwa anakupenda.
Women have many possibilities from 18 to 24 years, but from 25 and above, the graph starts to fall down whether they like it or not.
And Dear women, remember: we, men, love by reasons.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz