UNAPOAMUA KUINGIA PENZINI UWE NA MSIMAMO KWELI KWELI KWA SABABU MAPENZI NI KIFO: - EDUSPORTSTZ

Latest

UNAPOAMUA KUINGIA PENZINI UWE NA MSIMAMO KWELI KWELI KWA SABABU MAPENZI NI KIFO:


Image may contain: 2 people, people smiling, people riding bicycles and outdoor
Kaka Elista Mimi naitwa Erick kwa uhalisia wa stori yangu siwezi kuanza sasa nikamaliza leo ila naomba niseme kwa ufupi lakini naamini utanielewa na kujua kwamba KWANINI MAPENZI YANAUA?
Mapenzi hayaui mmoja mnaweza mkafa wote ama kwa wakati mmoja au kwa nyakati tofauti lakini ikawa VIFO VYENU BIMEBEBWA NA PENZI LENU WENYEWE.
Nimemaliza chuo ndo kwanza niko kuhangaika kutafuta kazi, Katika kupita pita huku na kule nikajikuta namba yangu nimeitawanya bila kujua, Kama bin adam nikaanzisha uhusiano na dada mmoja ambaye nilikutana nae moja ya fukwe za bahari hapa jijini Dar-es-salaam, Nilipendelea sana kupunga upepo maeneo ambayo niliweza kuona watu wakitafuta MAPUMZIKO kupitia upepo mwanana, Nilikutana na Juliana tukaingia uhusiano ambao kwa hakika NILIUFURAHIA SANA.
Mimi nilikuwa single, Juliana alikuwa single, Kwa pamoja tulifurahia uwepo wa kila mmoja, Shida ilikuja wakati ambao sikutarajia penzi letu lilikuwa tamu ajabu, Nikawa napokea simu za watu mbali mbali wakitaka kukutana nami kwa usaili nami niliamini hivyo, Mara moja nilikwenda kukutana nao lakini kila mmoja aliyeniona aliweka akili yake kwangu, Sikuwa Mtanashati lakini najijua NIKO HANDSOME.
Juliana alikuwa Mwanamke mwema na mwelewa sana hakuna siku hata moja alihoji simu niliyokuwa napigiwa zaidi neno lake moja tu ndilo lilitoka kinywani mwake;
"Darling take care"
Mwanzo nilijua ni haki yake Juliana kutaka usalama wa penzi lake, Lakini baada ya kuanza kushawishika na baadhi ya watu walioniita kwenye saili kwa ajili ya maombi yangu ya kazi, Kila Juliana aliposema "Darling take care" ndipo niliona kosa ndani yangu, Kwa sababu Juliana alifua nguo, alipasi na kunipangia rangi za kuvaa kila nilipokuwa nikienda huko alikoamini ni kwenye USAILI na kumbe tayari akili yangu ilikuwa ishabadilika na kuwa na mtazamo HASI.
Juliana alikuwa Msichana ambaye HAKUWA na ELIMU lakini alijaaliwa upana wa FIKRA kiasi aliweza kunipa changamoto kubwa, Kila nilipokuwa nikitunga UONGO ama kupanga KUCHEPUKA Jully alibaini lakini kwa HEKIMA alizojaaliwa na MOLA WAKE hakutaka vita bali alisisitiza "Darling take care" kwa tafsiri ya UPENDO WA JULIANA ni;
"MUOMBEE MEMA ADUI YAKO AISHI MIAKA MINGI ILI MUNGU ATAKAPOKUWA AMEKUKOMBOA AJIONEE VILE MUNGU AMEFANYIKA BARAKA KWAKO"
Maisha yangu na Juliana yalikuwa ya kuunga unga sana, Lakini baada ya kuanza kukutana na WASAILI wangu ambao walikuwa wanawake wenye nafasi zao kwenye ofisi ambazo niliacha namba kwa ajili ya taarifa yoyote ya nafasi za kazi.
Juliana alianza kunishitukia kwa sababu nilianza kuficha simu yangu, nilikosa ujasili wa kuacha simu kama nilivyokuwa naacha mwanzo, Tayari niliishaingiwa tamaa ya MAISHA kupitia wanawake ambao nilikutana nao Kwani kila mmoja na namna alivyonihitaji alinipa ahadi na matumaini na hayo ndiyo yalinivunjia UAMINIFU kwa Juliana, Ni kweli kabisa JULIANA alinipenda nami nilimpenda lakini kama kijana ambaye nimesoma lakini sipati kazi halafu nikiwatazama watu ambao walishindwa mitihani na KUTOENDELEA na Elimu ya juu wametusua maisha ukweli nilikuwa naugulia MOYONI.
Kesi na MIGOGORO isokwisha baina yangu na Juliana haikukomea kwenye MANENO tu lakini ilifika mahala TULIPIGANA KABISAA
Kuna siku nilijikuta nimemuumiza na kujutia Kwanini nampiga mtu ambaye anapambana kunisahihisha na kuniweka kwenye UAMINIFU?
Tayari akili imeegemea kwenye TAMAA YA MAISHA pamoja na kuumia lakini sikuona woga kuendelea na yaliyokuwa yanatugombanisha, Juliana alianza kukata tamaa TARATIBU japo sikujua Kwani hakunionyesha kama anabadilika zaidi alizidisha kunilinda japo alijitenga na VITA
Nikajikuta nimekuwa na wanawake wanne kwa wakati mmoja, Kila mmoja nilimpangia siku na muda wa kukutana nae, yalikuwa mahusiano ya maslahi sikwenda kutumika BURE⛔
Nilijitahidi kuwachuna pesa japo sikutaka Juliana ajue kama nina pesa, Juhudi ya kutafuta kazi wala sikuwa nayo tena bali nikawekeza akili yangu kwa wanawake hao kwa sababu waliweza kunipa pesa ya kukidhi mahitaji yangu, Siku zilivyokuwa zikiendelea Juliana wala hakutaka kujua nitatoka na kurudi saa ngapi zaidi alipenda kuuliza;
"ERICK UTAKULA NYUMBANI NIKUBAKISHIE CHAKULA?"
Nilijihisi unyonge hata kumjibu lakini nikiendelea na kilichokuwa mbele yangu, Na nilipokubari kwamba NITAKULA aliweka chakula, Lakini kwa kuwa nilikuwa na OUTING ZANGU KUNA WAKATI NILIRUDI NYUMBANI NIMEKULA hicho kitu kilimuumiza sana Mke wangu, Japo hatukuwa tumefunga ndoa lakini Juliana aliishi nami kwa heshima ya MUME nami nilifanya hivyo japo Tayari sikuwa MWAMINIFU kwake, Niliweza kujichanga pesa mpaka nikanunua gari, Hapo ndipo nilijua kwamba MASIKINI WANAFAIDI ZAIDI MAPENZI KULIKO WATU WENYE UWEZO😂😂
Unajua hakuna Mtu anapenda MAISHA MABAYA ila yanapokuwepo haimaanishi uyakane ama kuyakimbia bali unajivika nguvu ya kuendelea mbele huku ukitumainia kwamba ikosiku moja MUNGU ATATIMIZA NDOTO ZAKO👏🏼
Nina amini Mtu mwenye akili timamu anayo MAONO na hayo ndo humfanya kujibidiisha ili kufikia Malengo yake, Nikafika nyumbani na gari🚘 zuri na mtumba ambao haujatumika sana huko JAPAN🇯🇵
Juliana alikuwa busy na kufyeka majani nje ya nyumba tuliyokuwa tumepanga, Nilitegemea angelikuja kwenye gari ili ajue ni la nani lakini hakuacha kufyeka majani, Nikashuka kwenye gari na kumsogelea, JULIANA MPENZI WANGU MBONA HUJATAKA KUNIPOKEA KAMA ULIVYOZOEA?
Alitabasamu kisha akanipa HONGERA kwa kuendesha gari kwa siku hiyo, Akaniuliza;
"Erick wangu ulitaka nifanyeje pale?"
Niliumia kama bin adam na nikajikuta nasikia hasira Kwani Juliana alionyesha kunipuuza, Nikamuacha pale nje nami nikaingia ndani, Nikakutana na usafi wa hali ya juu, Mezani pana chakula kizuri na kinavutia nikasahau yote, Nilikuwa nina njaa nikaketi kula, Wakati naanza kula Mke wangu Juliana akaja ndani na kusema SAMAHANI SIKUKUNAWISHA MIKONO BWANA WANGU
Kauli ile ikaniuma ni kama Juliana alikuwa na dukuduku MOYONI ila hakutaka kulionyesha kwa paji ya uso wake, Nikamjibu Asante Mpenzi nilijua upo busy nami nikajipa majukumu yako ila Mke wangu Leo umeniamulia ASANTE nilikuwa nina njaa, Ila Juliana nipongeze Mke wangu tumepata GARI🚘 yale mateso ya kudandia Daladala🚌 ndo tumeyaaga, Erick mpenzi wangu NILIKUPENDA UKIWA UMEPAUKA BAADA YA KUTOKA KUTAFUTA KAZI leo nimeishi nawe hujafika kwetu, Unaongea na WAZAZI wangu na kila mara unawaahidi kwenda kujitambulisha, Lakini Mimi nimeongea na wadogo zako tu na ahadi yako kubwa kwangu SIKU ISIYO NA JINA UTANIPELEKA KWENU.
Leo gari inaanzaje kunipa FURAHA wakati najua sijawahi tembea kwa mguu? Maana hata Daladala ni gari, Ikiwa tuliweza kupata hela ya kupanda Daladala ilitosha sana kuona Iko siku tutanunua la kwetu, Ila Mimi sipo tayari hata kulipanda hilo gari Kwani ninajua ni juhudi za wanawake wenzangu😭😭😭😭
Ninachojua NAKUPENDA KUTOKA NDANI YA MOYO WANGU na nitasimamia nadhiri niliyoiweka na MUNGU WANGU KWAMBA ERICK AWE MUME WANGU usione niliacha kukulalamikia ukadhani maumivu yaliisha⛔
Ninaumia zaidi Leo kuona Kuna Mwanamke ameweza kukupa GARI wakati huo Mimi siwezi hata kukununulia baiskel😭😭 lakini ninajua ZAWADI YANGU KWAKO NI ADHIMU NA NI YA KUDUMU labda nikwambie Mimi nitakufumba macho ukifa lakini UTAISHI MAISHANI MWANGU KAMA MUME wala sintojaribu kukusaliti hiyo ndiyo ZAWADI NAKUPATIA.
Gari utalitumia kwa usafiri lakini ukirudi nyumbani utanikuta nakungojea kukulinda na kukutetea kwa moyo wangu wote, Najua kwa sasa umegawanya UPENDO WAKO kwamba Mimi Kuna unachonipendea, Lakini Kuna mwingine ama wengine nao unawapenda kwa sababu ulizo nazo kwao😭😭😭
Mimi naomba nitamke kwa mamlaka ya kinywa changu HILO GARI SINTOLIPANDA NIKIWA HAI na kama UTANIPANDISHA NIKIWA NIMEKUFA BASI LAANA IWE JUU YAKO.
Basi Juliana nimekusikia, usiendelee kusema maneno magumu kama hayo, Naomba yaishe nimekuelewa ila ujue tu NIMEPAMBANA KUPATA GARI HILI wala sio kama unavyofikiria.
Erick huna kazi, hutafuti kazi kumbe hilo GARI limepatikana kwa muujiza? Rafiki wewe tuyaache maisha yaendelee nitakapoona nimechoka kushuhudia haya NITAKUAGA KWA WEMA KABISA wala siwezi kutoroka nadhani Swala la Mimi kuwa pamoja maishani litafikia kikomo hapo but UTAISHI NAMI MOYONI.
Kwa ujumla ile FURAHA ya gari pamoja na chakula nimekula wala sikutaka kujua radha yake, Moyo uliniuma sana nikakumbuka andiko kwenye BIBLIA;
"JIBU LA UPOLE HUNENEPESHA MOYO"
Ila Juliana aliukondesha MOYO WANGU kwa maneno ya upole, Sikutaka kuendelea kuzungumzia gari tena nikajibalaguza mara nikasikia sauti mororo "ERICK NJOO UOGE" Unajua niliishiwa pozi Kwani nikajionea maana ya neno lililoandikwa kwenye maandiko matakatifu;
"NI NANI AWEZAYE KUMUONA MKE MWEMA?"
Mimi nikamuona ni Juliana, nikajutia sana, niliamini Upambanaji wangu mpaka kupata GARI ungemfurahisha Mke wangu lakini ndo kwanza naona HEKIMA ZAKE huku akikataa kata kata kushiriki NAJISI ILE😭😭😭
Niliinuka nikaenda kuoga lakini nilikuwa mwingi wa majuto pamoja na kuona hakuna nililofanya, Japo nikajiapiza kuwaacha wanawake wale japo nibakie na mke wangu pengine taratibu angenielewa, akilini nilijidanganya kwamba JULIANA ALIKUWA NA WIVU na taratibu utamuisha na atalipanda gari ila itachukuwa muda.
Siku zilisonga na maisha kuendelea, Kusema ukweli nikapambana kutafuta kazi nikapata kazi katika kampuni moja hapa jijini Dar-es-salaam sikulipwa mshahara mkubwa lakini ulitutosheleza na maisha yakasonga, kikwazo ilikuwa pale natakiwa kutoka na Mke wangu lakini alisimamia msimamo wa kutopanda gari hilo, Huko nje kwa wale wanawake walijitahidi kunibembeleza ili niwe nao kwa kuamini nimeanza kiburi, Lakini sikuwajali Kwani nilijiapiza kutokuwa nao, Kati ya wale wanawake mmoja alikuwa na MUME na wakati wa uhusiano wangu na yeye alijikuta amemdharau sana mumewe, Kiasi kwamba yule Mwanaume akaanza kumfuatilia mkewe, Wakati anakuja kujua Mimi tayari nimeachana na mkewe, Lakini hakujua hilo na badala yake HASIRA zake akazielekeza kwangu, Alianza kutafuta kujua maisha yangu na kwa namna fulani alifanikiwa, Wakati hayo yakifanyika Mimi napambana na Mwanamke wake kumkataa wala sitaki hata kuonana nae, Nae alianza kunitishia kwamba atahakikisha ananivunjia ndoa yangu, Lakini sikujali Kwani Juliana aliisha anza kunielewa kwamba nilimsaliti nikajutia na sasa nipo kwake tu japo kikwazo ilikuwa gari ila nilipanga kuliuza ili ninunue jingine, Siku moja mke wangu akanipigia simu Kuna mtu amemfuatilia kutoka sokoni mpaka nyumbani, alikuwa ni Mwanaidi Mwanamke ambaye ndiye aliyeniahidi kupambana nami, Mimi nae wakati narudi nikaona pikipiki imebeba mtu inanifuatilia mpaka nyumbani, Basi jioni hiyo tukawa tunapanga namna ya kukabiliana na usalama wetu, ilibidi niwe mkweli kwamba yule ni Mwanaidi ndo mwanamke alokuwa hawara yangu, Juliana alinielewa sana na kuniambia nisiogope NDOA YETU NI IMARA MNO wala haiwezi kusambalatishwa na Mtu ⛔
Siku zilipita kama tano, Nikawa natoka nyumbani kwenda kazini njiani nikagundua gari langu lina pancha ndipo nikaegesha pembeni ili nibadili tairi Kwani nilikuwa ninalo tairi la ziada, Ghafla ikaja gari nusu inigonge halafu jamaa akasimama mbele yangu, alishuka na kuniomba msamaha nami nikamkubalia, Jamaa aliondoka nami nikaendelea na kazi iliyokuwa mbele yangu, Nilipofika ofisini nikamsimulia mke wangu akanipa pole na kuniuliza MUME WA MWANAIDI unamjua? Nilisema hapana, akaniambia kwa sasa unatakiwa umjue Kwani huwezi jua pengine nae Mwanaidi alimuumiza MUME wake na sasa wameridhiana wewe ukaliliwa wivu na MUME WA MWANAIDI na Mimi nikaliliwa wivu na MWANAIDI sote tunakuwa kwenye RISK
Ni kama Juliana alinitoa usingizini Kwani nikajikuta nawaza mengi sana, Lunch time nilikutana na Yule bwana alotaka kunigonga, nikajikuta nakuwa mwingi wa mawazo, Nilikula kwa makini lakini nikajiapiza kumfuatilia nijue ni nani? Alipoondoka aliniacha nikiwa nazogoa wa WAFANYAKAZI wenzangu ndipo inanifuatilia lakini ghafla gari lake lilipotea Kwani bodaboda wangu tulipofika jangwani alisema mjini haingii, Basi nikarudi nae mpaka ilala Kwani ndiko ofisi zangu zilikuwa, Muda wa kuondoka kazini uliwadia nami nikajiandaa ili nielekee nyumbani, Nilinyoosha mpaka nyumbani na nilipofika nyumbani nikashuka kwenye gari wakati natembea kuelekea mlango wa nyumbani kwangu nikasikia mtu ananiita, Kigeuka ni jamaa alivaa mask na ameshika bunduki mkononi, Nikageuka kukimbia niingie ndani nikapigwa risasi mbili moja begani na moja kwenye paja Tayari majilani waliishaanza kumfukuza mtu yule mbele alipaki pikipiki akadandia na kutokomea, Nimelala sijitambui, sijui lolote zaidi nikajikuta nipo hosp na Juliana wangu, Nililia sana kuona Pengine ningekufa nikamuacha MPWEKE mke wang😭😭😭
Nikapata nafuu na kutoka hospitali, Nikawa siwezi kutoka tena mkewangu alinisimamia na kunipa care za ajabu kiasi kwamba NIKAJIAPIZA NIKITOKA KITANDANI MWANAIDI ATANITAMBUA Kwani niliishajua kama sio yeye Basi ni MUME wake walitaka nife, Siku moja nikaita dalali akalibeba gari akaliuze ili nikipona ninunue gari jingine, Gari likauzika na nikaendelea kutibu Majeraha yangu, Siku moja mke wangu akawa ametoka kwenda duka la dawa wakati anarudi akakutana na Wanawake wawili wakaanza kumchangia na kumpiga sanaa😭😭😭
Muda ukaenda sana Juliana harudi na simu yake haipatikani, Ndipo nikapata msg kwamba Mke wako yupo hapa Hosp na ana majeraha mkononi, Pamoja na MAUMIVU na vidonda vya risasi niliinuka nikajitia ujasili na kwenda nje ndipo nilipata jilani yangu nikamuomba msaada wa kunifikisha hosp na alinikubalia na nilipofika hosp nikamkuta Mke wangu anatabasamu kuniondoa wasi wasi lakini tayari nimejua mwenzangu ananipa moyo tu, Nilimuuliza Juliana;
"Mke wangu watu walokushambulia wapoje?
Juliana alisema sikuwajua mwanzo ila mwishoni mmoja aliita Mwana twende Kuna watu wanakuja, Nilisikia uchungu sana kiasi kwamba NIKATAMANI NIMFUATE MWANAIDI ili akaniue ama Mimi nimuue Kwani tayari nimejua ndiye aliyetaka nife😭😭😭
Mke wangu aliishajua ninachiwaza akaniambia ERICK HUKUFA KWA MPANGO WA MUNGU vivyo hivyo sijafa kwa uweza wa MUNGU maana walidhamilia kuniua Kwani wamenikaba sana, Just relax Mimi niko imara sana, hatupashwi kuwazia MALIPIZI bali tunajukumu la kumuomba MUNGU adui zetu apigane nao.
Daktari alikuja akamruhusu Mke wangu na kumpatia madawa ili apone, Jilani yetu alikuwa pamoja nasi akitupa FARAJA kwa tunayopitia, tulirudi nyumbani na tulipata TAKE AWAY na tukala na kupumzika, Kesho yake niliamka nikamwambia mke wangu tunapaswa kuhama pale lakini alikataa na kuniambia nipone kwanza, Siku ziliendelea na majeraha yangu kupona nikarejea kazini, Siku moja nikiwa naangalia TV ofisini nikaona BREAKING NEWS Mume amuua mkewe nae ajiua, Ni wakazi wa MBWENI kwa majina yao ni MWANAIDI pamoja na mumewe JAMAL ndipo zikatokea picha zao, Ni Mwanaidi yule niliyemjua lakini Mumewe ndiye yule bwana alitaka kunigonga kwa gari, ikabidi nimwambie mke wangu akasema ataangalia taarifa ya Habari, Nikajisemea ki MOYO MOYO ina Maana Mimi aliyekuwa anataka kuniua ni Mume wa Mwanaidi? Na Mwanaidi alitaka kumuua Mke wangu? Nilifadhaika sana na nikajikuta najutia sana kumtendea niliyomtendea mke wangu, Juliana alikuwa Mwanamke mvumilivu sana lakini pia ALINITII kama impasavyo mke kwa MUME wake.
Maisha yetu yakawa mazuri sana, Tulifunga ndoa na kubarikiwa watoto mapacha ambao niliwaita MICHAEL NA GABRIEL👏🏼

Ndugu zangu mlioweza kusoma historia yangu napenda mjue NIMEPUNGUZA MENGI ili nisimchoshe Elista, But MUNGU hakuwa mjinga kuuliza;
NI NANI ALIYEMUONA MKE MWEMA?
Napenda mjue kwamba Mimi Erick nimempata MKE MWEMA👏🏼
Bila Juliana kusimama kulitetea penzi letu leo ASINGEKUWA MKE WANGU na nikiri kabisa kwa mwendelezo nilokuwa nao pengine leo NISINGEKUWEPO DUNIANI maana kwa uchache wa ujinga nilofanya nimenusurika kufa mara 3😭😭
Namtukuza MUNGU KWA AJILI YA JULIANA lakini pia nasema ASANTE KWA MUNGU WETU KUTULINDA MPAKA LEO👏🏼

Pole sana Erick, Hongera sana Juliana, Kwa hakika umemkomboa Mume wako, Umetimiza andiko la ABIGAIL na MUNGU atakupa BARAKA WEWE NA UZAO WAKO👏🏼
Niseme tena;
UNAPOAMUA KUWA PENZINI UWE NA MSIMAMO KWELI KWELI KWA SABABU MAPENZI YANAUA nataka nikumegee maana ya neno langu kupitia andiko linalopatikana kwenye kitabu cha WIMBO ULIO BORA 8⤵
6. Nitie kama mhuri MOYONI mwako, Kama mhuri juu ya mkono wako, Kwa Maana UPENDO una NGUVU kama Mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni Mwako wa MOTO. Na miali ni miali ya YAHU"

Mungu awakomboe watu wote wenye MAPENZI YA DHATI KWA WENZA WAO ikiwa Kuna unafiki na siri Basi AMKOMBOE ANAYEDHURUMIWA HITAJI LA NAFSI YAKE👏🏼
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz