UNAJUA KWANINI MAPENZI HAYALAZIMISHWI? - EDUSPORTSTZ

Latest

UNAJUA KWANINI MAPENZI HAYALAZIMISHWI?

Image may contain: 1 person, sitting
Kwanza ujue kwamba UPENDO ni muingiliano baina ya MOYO NA NAFSI kwa uhitaji wake, Hitaji linalotokana na MOYO kuna uhakika kwamba NAFSI imeridhia na ndo maana HUWEZI KUKWEPA MAUMIVU YA MAPENZI IKIWA NAFSI IMEMTAJA MTU HUYO🙏
Kupenda ni jambo moja na kupendwa ni jambo MTAMBUKA kwamba ni ngumu kuhakiki japo unaweza kuaminishwa, Hakuna jambo GUMU na lenye uzito usobebeka kama KUMPENDA ASOKUPENDA💔
Tayari ushampenda na unatamani awe wako, Lakini Kuna ambalo amekujenga hata ukazama kwenye penzi lake JE KWANINI UNATUMIA NGUVU NYINGI KUMFANYA AKUPENDE?
Maana UPENDO una tabia ya kuambukizana iweje wewe umpende na yeye hakupendi?
Usijiamini kwa uwepo wake kwako pengine zipo sababu zinazomfanya aendelee kuwepo, Wapo watu ni wavivu pengine anapenda huduma zako, Au ni hilo penzi unampatia ndo linampa mawazo kulikosa, Je kama ni HURUMA YAKO NDO ANAIWAZA KUIACHA?
Upendo wa upande mmoja una GHARAMA ndo maana sipendi kukuruhusu wewe ndo umpende peke yako, Raha kabla hujaonyesha UNAMPENDA Kuna ishara ya UPENDO wake kwako, Kuna raha KUPENDWA NA UMPENDAYE lakini ni fahari KUMPENDA AKUPENDAYE hapo ni kama switch na umeme Yaani ni kubonyeza tu MWANGA UNACHUKUWA HATAMU💡
Hakuna darasa la UPENDO bali tunashilikiana KUPENDANA ili UPENDO UTOWESHE UPWEKE na asikudanganye Mtu kuishi na asokupenda kwamba Kuna wakati atakupenda, UPENDO haujifunzi bali ni tendo la UTASHI.
Usilazimishe akupende bali MFANYE AKUPENDE ila ukiona hathamini UPENDO wako Basi mwache aende anakopenda yeye, Maana asokukuwa na UPENDO ni PUNGUANI ila aliye timamu ANALO PENDO KWA ALOCHAGULIWA NA MOYO WAKE kwa maana hiyo wewe HAKUPENDI
Ondoka kwenye penzi la UPENDO WA upande mmoja ni HASARA KWAKO.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🕑
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz