UNAFIKIRI NI KWANINI WATOTO WA KIZAZI HIKI WANAHARIBIKA ZAIDI KULIKO WATOTO WA KIZAZI KILICHOPITA? - EDUSPORTSTZ

Latest

UNAFIKIRI NI KWANINI WATOTO WA KIZAZI HIKI WANAHARIBIKA ZAIDI KULIKO WATOTO WA KIZAZI KILICHOPITA?

Image may contain: 2 people

 Malezi ni msingi wa mtoto katika maisha yake ya baadaye, Kuna tatizo kubwa linatafuna familia nyingi na hasa wahanga wakuu katika tatizo hili ni zile familia zenye kulea watoto upande mmoja... Kwa vyovyote vile KAZI NA DAWA kwa hilo wala sipingani nalo kwani baba au mama ambaye yupo peke yake baada ya kuachika ama kufiwa ni lazima awe na TABIBU! Wazazi wengi hawajajuwa namna ya kuisimamia familia pindi wawapo peke yao na hilo huwasababisha kushindwa kuweka uwiano kati ya MAHUSIANO NA MALEZI KWA FAMILIA ZAO na hilo limeharibu watoto wengi sana, Mzazi wa kike Yaani MAMA ndiye aliye kwenye wakati mgumu sana pindi anaposhindwa kubalance Kwani HAKUNA KITU HUMUUMIZA MTOTO KAMA AKIONA MAMA YAKE ANABADILI WANAUME japo ni kweli kabisa hawezi kuishi bila mpenzi lakini busara inahitajika kuchagua mwanaume ambaye wanae watamjuwa na kama akiachana nae basi ni vyema akaishi kwa TAKE AWAY kuliko kila mwanaume anayempata ampeleke nyumbani kwake, Upande wa BABA mara nyingi hawalei watoto lakini ikitokea amelea peke yake Basi anawajibika kubalance vizuri juu ya MAHUSIANO YAKE PAMOJA NA MALEZI KWA WANAE Kwani nae asiposimama imara katika hayo huwayumbisha watoto na muda mwingine wanaangamia katika tabia mbaya Kwani baba muda wake kufuatilia watoto ni mdogo kutokana na majukumu ya kimaisha... Nje ya familia ipo JAMII nayo ni vyema kwa kila mzazi kuiangalia ili kuepuka yale ambayo yatamvunjia heshima, Upokeaji wa jambo katika JAMII huwa tofauti kulingana na uelewa wa kila mmoja na inaleta maana nyingi kwa wale wanaokuzunguka, Mwanamke akionekana kuwa na zaidi ya mwanaume mmoja huitwa MALAYA lakini kwa Mwanaume kuwa na zaidi ya Mwanamke mmoja huitwa MHUNI na ukizingalia maana za sifa hizi mbili unaambiwa Mwanamke HATOSHEKI ila kwa mwanaume ni KIDUME... Ni vyema kujiheshimu mwenyewe ili watoto wakuheshimu na JAMII itasema vile unajiheshimu.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz