UMEACHWA NA MTU UNAEMPENDA? HII INAKUHUSU - EDUSPORTSTZ

Latest

UMEACHWA NA MTU UNAEMPENDA? HII INAKUHUSU

No photo description available.

Ipo siku utakuja kukutana na mtu ambae atakufanya usahau maumivu yote ya mapenzi ambayo umepata kukumbana nayo. Ambae atakufanya uwe na furaha Ambae atakuja na kukupenda pasi na kikomo licha ya hali ulionayo. Utakuja kumpata ambae atajivunia kuwa na wewe na kuwa tayari katika mahusiano na wewe. Ambae atakubali kubeba madhaifu yako. Pia atakuwa na hofu ya kukupoteza na hatatumia past yake kukuadhibu wewe! Na atakuwa kila kitu kwako. Najua utaona kama uongo tu na kujifariji lakini nakuomba niamini siku moja utampata mtu huyo muhimu kwako ambae atakuwa wako peke yako. Mungu tayari anae huyo mtu kwa ajili yako na anasubiri wakati muafaka akupe mtu huyo. Acha kulia lia songa mbele. Kuendelea kulia na kulazimisha maji kupanda mlima ni kujipotezea muda wako wa kuwa na huyo mtu mtarajiwa wako. Kuwa tayari kumkumbatia huyo mtu atakapofika. Umeanguka katika mahusiano? Inuka kung'uta vumbi na songa mbele kukunjwa jamvi sio mwisho wa maongezi. Subira yavuta kheri
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz