UCHOVU ISIWE SABABU YA KUNYIMANA ‘CHAKULA CHA USIKU’ - EDUSPORTSTZ

Latest

UCHOVU ISIWE SABABU YA KUNYIMANA ‘CHAKULA CHA USIKU’

No photo description available.
Ndani Ya Maisha Ya Ndoa, Muda Wowote Mwenzako
Anapohitaji Penzi Hutakiwi Kumkatalia Kwa Kuwa Wewe
Ndiye Daktari Wake Na Kumkubalia Kwako Ni Sawa Na
Kumtibu Ugonjwa Ambao Ungeweza Kuyaathiri Maisha Yake.
Hata Hivyo, Asilimia Kubwa Ya Wanandoa Wanatajwa
Kufanya Tendo La Ndoa Wakati Wa Usiku. Usiku Wa Saa
Ngapi? Hiyo Itategemea Na Wanandoa Husika.
Lakini Sasa Inaelezwa Kuwa Wanandoa Wanaofanya Kazi Ni
Vigumu Sana Kulifurahia Tendo La Ndoa Kwa Kulifanya
Usiku. Hii Ni Kwa Sababu, Muda Huo Kila Mmoja Anakuwa
Amechoka Kutokana Na Mihangaiko Ya Siku Nzima.
Usiku Ni Tatizo?
Wanaume Wengi Wakati Wa Usiku Ndiyo Wanautumia
Kutafakari Juu Ya Maisha, Pia Ni Wakati Ambao Wanakuwa
Wamechoka Hivyo Wanaweza Kukosa Mshawasha Wa
Kukutana Na Wake Zao.
Ukijaribu Kufuatilia Utabaini Ndoa Nyingi Ziko Kwenye
Migogoro Chanzo Kikiwa Na Wanawake Kutopatiwa Haki Zao
Za Ndoa. Wanaikosa Haki Hiyo Kwa Kuwa Muda Ambao
Waume Zao Wanatakiwa Kuwapa ‘Mambo’, Wanakuwa Hoi.
Mbaya Zaidi Baadhi Ya Wanawake Hufikia Hatua Ya Kuhisi
Wanasalitiwa Kumbe Siyo Kweli Bali Inatokana Na
Kutopatiwa Raha Hiyo Kwa Wakati Walioutarajia.
Wataalam Wa Mapenzi Wanaeleza Kuwa, Usiku Ndiyo Muda
Muafaka Kwa Wanandoa Kukutana Na Kwa Mwanaume Hata
Kama Atakuwa Anajisikia Hali Ya Kuchoka, Ajue Ana Wajibu
Wa Kufanya Hivyo.
Kufanya Mapenzi Ni Moja Ya Mazoezi Hivyo Mwanaume
Anaporudi Nyumbani Asikimbilie Kuoga, Kula Na Kulala Bali
Akumbuke Kumpatia Haki Mke Wake, Haki Ambayo Pia
Inamsaidia Kimazoezi.
Inaelezwa Kuwa, Mwanaume Kujihisi Uchovu Kila Siku Na
Kushindwa Kufanya Tendo La Ndoa Ni Dalili Kwamba Ana
Tatizo La Kiafya Analotakiwa Kulitafutia Ufumbuzi Haraka
Kabla Ya Kuiathiri Ndoa Yake.
Mapenzi Ni Starehe
Ifahamike Kwamba, Kufanya Mapenzi Licha Ya Kwamba
Unatumia Nguvu Na Akili Lakini Ni Sehemu Ya Kustarehe.
Ndiyo Maana Wengine Baada Ya Kumaliza Shughuli Zao Za
Siku Nzima Badala Ya Kwenda Baa, Moja Kwa Moja
Wanakwenda Nyumbani Na Wakifika Huko Wakioga
Wanaweza Kutumia Muda Mwingi Kitandani Na Wenza Wao.
Kwa Maana Hiyo Kukutana Faragha Isichukuliwe Kama Kitu
Kitakachokufanya Uzidi Kuchoka Bali Kwa Kutumia Kanuni
Sahihi
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz