SOMA MKASA HUU, UTAJIFUNZA KITU. - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA MKASA HUU, UTAJIFUNZA KITU.

Image may contain: 2 people, people smiling

Siku moja Anita alimtazama mama yake kisha akamuuliza, "Hivi mama una miaka mingapi?" mama yake alistaajabu kuwa nini kimemsibu mwanae hadi kumuuliza swali lile ila akaamua tu kumjibu, "Nina 35 mwanangu, kwanini umeniuliza hivyo?" Anita alistaajabu kwa jibu lile la mama yake kisha akaendelea akamwambia, "Hakika nashindwa kuamini mama maana hakika nikikuangalia kila siku unazidi kupendeza na kuonekana msichana mrembo yani kama dada maria anaesoma darasa la mbele yetu, yani la 7.
Ningependa leo na mimi unipe siri ya mafanikio yako ili sura yangu idumu kuwa nzuri hadi nikiwa mkubwa nisijezeeka mapema, nikikua mkubwa mmama nataka niwasimulie watoto wangu nami siri hiyo nzuri".

Mama yake alimpa jibu kuwa, "Siri kuu ya amani na furaha yangu ni UTULIVU WANGU daima sina kinyongo, bifu, ugomvi wala chuki na mtu, yeyote anaeniudhi humsamehe na kutabasamu, daima namuachia Mungu yale yote nisemwayo vibaya sina mda wa kusutana wala kugombana ndio maana hata baba yako siku tukikosana akianza kunifokea huwa namkalia mbali utanikuta nimepoa naendelea na kazi zingine hadi mda akitulia kisha ndipo namkarimu tunayamaliza kwa amani na upendo kila mtu anasahau hata kama siku hiyo tulikorofishana.

Moyo wangu daima umejaa amani na furaha mwanangu sina mda wa kuwaza ugomvi,visa, kusononeka au matatizo, iwapo mambo yetu yakiwa mabaya sana tukiandamwa na matatizo makubwa ninachofanyaga ni kupiga magoti nasali na kumkabidhi Mungu, hakika nikimaliza kusali najikuta amani yangu imejaa tele hata kama dhiki bado ipo ila ninatumaini Mungu amesikia maombi yangu na ipo siku mambo yatatulia".

Machozi ya furaha yalimtoka Anita kutokana na maneno yale mazito aliyoambiwa na mama yake hakika siku hii alijua SIRI YA KUTOZEEKA MAPEMA ni kuishi maisha ya tabasamu na watu wote, kuepuka migogoro isiyo ya lazima, kuepuka kukata tamaa, kuepuka manung'uniko, ugomvi, chuki na hasira.

Nami leo wewe unaesoma post hii ninaukabidhi mwaka wako ujao wa 2017 ukawe mwaka wako wa pekee Mungu akupe maisha ya amani na furaha yaliyojaa tabasamu, uishi vyema na mume wako, mke wako, watoto wako, ndugu zako Na majirani zako, upendo utawale kati yenu na mafanikio yaujaze mwaka wako wa 2017 kila utakalolifanya likafanikiwe Mungu akubariki na kukulinda akuepushie majanga yote, Amani na furaha vitawale ndoa yako, vitawale kazini kwako, vitawale biashara zako, vitawale afya yako, vitawale elimu yako, vitawale maisha yako ulalapo na uamkapo.

Kama unakubaliana nami sema AMEN kisha hakikisha una SHARE post hii.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz