PENZI LA DHATI LIKO HIVI...! - EDUSPORTSTZ

Latest

PENZI LA DHATI LIKO HIVI...!

Image may contain: 2 people

UPENDO WA DHATI HUSIMAMIA PENZI LA AWALI ambalo mtu aliufundisha moyo wake juu ya kumpenda mwenzie... Ukiona umependwa na mtu ambaye alishampenda mtu huko nyuma Basi ujue UMEPATIWA UPENDELEO ili kuulinda moyo wake, Nimekutana na kesi nyingi zinazohusu NDOA na MAHUSIANO kwa ujumla ya kuwa "MWENZA HANA TENA LILE PENDO ALIONYESHA WAKATI WAKIKUTANA" Kaka mmoja na Dada mmoja waliingia katika mahusiano ya muda mrefu ambayo yaliwapelekea kupata mtoto, wawili hawa walipendana sana japo walikuwa wanakumbana na changamoto ya wazazi wa pande zote mbili, Upande wa Mwanamke hawakuwa wanajiweza hivyo mpango wa familia hiyo walipanga binti yao aolewe na familia yenye uwezo japo tayari binti aliisha zaa, Upande wa mwanaume wao waliyazoea maisha na kijana wao alikuwa mwalimu hivyo kabla ya kijana wao kuzaa na binti huyo walipanga mtoto wao ampate mwanamke msomi kama kijana wao, Vikwazo hivyo havikuathili penzi la wawili hawa maana tayari wao walishapendana! Mtoto wa wapenzi hawa alipofikisha miaka 4 kule kwa binti akaenda mwanaume kumposa binti Huyu bila yeye kujuwa na baba mzazi wa binti alipokea posa ile Kwani malengo yake yalitimia kutokana na posa kuletwa na familia ya kitajiri, Binti akapewa taarifa na kuambiwa siku atakayokuwa anafunga ndoa lakini alishindwa namna ya kuwakatalia wazazi wake na pia akashindwa kumwambia mzazi mwenzake alibaki akiumia asione msaada katika hili... Siku ya harusi ikafika binti anatakiwa kwenda kwao na ilizoeleka kila wakitaka kutembelea wazazi waliambana na mtoto wao swali likamjia binti NAAGAJE? Ikambidi ajikaze tu akamwambia mzazi mwenzie ambaye pia ndilo penzi la usichana wake kuwa anakwenda nyumbani lakini wakati akimalizia kusema akabubujikwa na machozi kitu ambacho kilimuumiza sana mwenzie na akamsogelea ili kujuwa kwanini analia huku mtoto nae akaanza kulia kuona mama yake analia kwa hakika kijana Huyu akawa katika wakati mgumu asijue sababu... Binti akagugumia kwa uchungu akasema "BABA AMEPOKEA MAHALI NAENDA KUOLEWA LAKINI WEWE NDIYE PENDO LANGU LA KWANZA ILA NAOGOPA NISIJE KOSA RADHI YA WAZAZI" Kijana aliishiwa nguvu, kulia anashindwa akabaki anamuangalia mpenzi wake, Aliyemfuata tayari anaanza kumuita binti, Binti anaanza kuondoka huku analia, kijana analia na mtoto wao analia kwa uchungu, Kijana hana tena pingamizi lakini akasikika akisema "MIMI NITAUMIA MWISHO WA SIKU NITAZOEA LAKINI NAUMIA ZAIDI JUU YA MTOTO WETU" Binti akamwambia mzazi mwenzie naomba mje harusini... Gari likaondoka na binti huku akiwaacha mzazi mwenzie na mtoto wakilia kilio cha msiba, Kijana akabeba mwanae wakaelekea kwenye harusi walipofika baba wa binti alipomuona kijana akamfuata na kumwambia aondoke haraka lakini binti alishaona hilo akamwambia baba yake ikiwa mzazi mwenzie ataondoka Basi yeye atajiua, Binti karata yake ya mwisho ilikuwa akisubiri huruma ya muoaji Kwani kwa vyovyote vile lazima atashitukia, Muda wa bibi harusi kuingia kanisani ukawadia taratibu akikanyaga kwa madoido huku vigeregere vikisikika na maua yakimwagwa mahala anapopita, Bwana harusi akishuhudia mkewe mtarajiwa akiingia mahala patakatifu ili wafunge ndoa, Bwana harusi akapewa jukumu la kuifunua shera ili amtazame mkewe ghafla akakutana na uso ulojaa machozi bibi harusi analia bila kunyamaza, Bwana harusi akauliza UNA TATIZO GANI? Bibi harusi akainua kichwa na kutazama kushoto walikokaa wageni waalikwa akakutanisha macho na mzazi mwenzie wote wakilia pamoja na mtoto wao, Bwana harusi alishabaini kinachoendelea kuwa Kuna siri hajaijuwa ikabidi amuulize tena bibi harusi NIJIBU UNALILIA NINI? Bibi harusi akajibu kwa kwikwiiiii "NINA MTOTO NA PIA NIMEZAA NA MWANAUME NIMPENDAYE JAPO WAZAZI WANGU HAWAKUMPENDA" Bwana harusi aliumia sana na alipeleka macho yake tena kwa Kijana yule alozaa na bibi harusi kijana analia muda wote, Baba wa binti akashituka na kuwasogelea maharusi wale kabla hajasema neno Bwana harusi akapaza sauti na kusema "NAKUOMBA RAFIKI YANGU USIONDOKE! Maana kijana yule alishaanza kuondoka kwakujuwa ishakuwa hatari ile, Kijana akasogea waliko maharusi lakini akiogopa sana aliposogea Karibu yao bwana harusi akamwambia bibi harusi NENDA KWENYE PENDO LAKO LA DHATI... Bibi harusi haamini kile anakiona na kukisikia, Bwana harusi akamshika mkono na kumpeleka kwa mzazi mwenzake na kuwaambia leo ni ndoa yenu wala si yangu, Bwana harusi akasikika akisema JAMANI MTANIWIA RADHI NILITAKA KUDHURUMU PENZI LA WATU nawaomba mniruhusu kutamka rasmi Mimi nimesindikiza harusi hii na muoaji ni Huyu huku akimgusa kijana yule, Ukumbi mzima umebaki unashangaa! Harusi ikafungwa kwa Kijana huyo na binti yule ambaye tayari alikuwa bibi harusi... Ujumbe huu unafundisha nini? UKIMTUMAINIA MUNGU KILA JAMBO NI JEPESI.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz