NJIA ZA ASILI ZA KUONDOA MIKUNJO USONI. - EDUSPORTSTZ

Latest

NJIA ZA ASILI ZA KUONDOA MIKUNJO USONI.
kumekuwa na dhana kwamba uwepo wa vipodozi vya kuondoa mikunjo ya ngozi ni wa miaka ya hivi karibuni, la hasha ukweli ni kwamba krimu za kuondoa mikunjo zilitengenezwa kwa mara ya kwanza huko Misri enzi hizo.

kuna njia rahisi sana ambazo zina uwezo wa kutatua tatizo la mikunjo bila kuhaha katika maduka ya vipodozi kutafuta losheni au vipodozi ili kukabiliana na tatizo hili. Sasa unaweza kutumia vitu vya kawaida kabisa kuondoa mikunjo kwa urahisi na kuufanya uso wako uonekane kijana zaidi. Baadhi ya njia hizi ni kama;

Kutumia tango,yai na limao
vijiko 2 vya juisi ya matango
ute mweupe wa yai
kijiko kimoja cha maji ya limao

Maandalizi:
changanya vitu hivyo kwenye chombo kimoja na hakikisha kwamba vitu vyote vimechanganyika sawasawa. Hifadhi mchanganyiko huo tayari kwa kuupaka kwenye uso.TANGO


LIMAO


UTE MWEUPE WA YAI
Jinsi ya kutumia:
osha uso wako kwa maji na sabuni na hakikisha umeukausha baada ya kuosha uso wako
pakaa mchanganyiko wako ulioandaa kwenye uso wako na acha mchanganyiko huo bila kunawa kwa muda wa dkk 15 hadi 20 kabla yakuosha uso wako
osha uso wako kwa kutumia maji ya uvuguvugu
 To be continued............

ENDELEA KUTEMBELEA UKURASA HUU KWA MUENDELEZO WA DONDOO ZA UREMBO ASILIA !!!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz