πŸ’–πŸ’–NDOA NA ZAKHMA*πŸ’–πŸ’– - EDUSPORTSTZ

Latest

πŸ’–πŸ’–NDOA NA ZAKHMA*πŸ’–πŸ’–


Image may contain: 2 people, people smiling, people standing
Ndoa za Zamani zilidumu unajua kwanini...!? ~Jana nilikuwa faragha na babu nikamuuliza hivi inakuaje!!? Akaniambia,'Mjukuu wangu! Zama zetu tulikuwa kila uchao tukizindua kijisababu japo kidogo kuifurahisha mbavu Yako ila zama hizi mnatafutiana vijisababu vidogo vidogo kuibua migogoro.. Na daima ukichakura kinyesi lazima kitoe harufu tu...!" Dah..! Nilijisawazisha kisha nikachachawiza kujua zaidi, akasema; "Zama zetu hatukua na mahusiano kabla ya ndoa ila nyie tangia mvumbue masala kusubiri ya kwive mnaona mnachelewa... Tahamaki mkijakuoana hamkawiagi kuachana au mnabaki mkiishi kimazoea tu! Kila dakika kununiana bila sababu za msingi..!" Sikutaka kuuliza zaidi kila kitu kilikuwa bayana.. Ndipo nikasema sitofaidika mwenyewe ndiyo hizo hoja nimewaletea.. Kila mmoja akili kichwani mwake.. Nawaombea walio kwenye ndoa Allah Azihifadhi na Alinawirishe pendo lenu na wanaotarajia basi Allah Awape wenza wema... Amiyn ya Allah
*MAWADDAH. WA RAHMA*
πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ₯’πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz