Unajifanya ni Mama bora, unawapenda wanao na kuwapeleka shule nzuri, unahakikisha kuwa wanakula vizuri. Lakini una binti wa kazi, kila siku ni kumtukana, unamnyanyasa na kama ni chakula hali meza moja na wewe, unamuona binti wako wa kazi kama choo;
(1) Huna akili, kwani kama kweli unawapenda watoto wako, lakini binti wa kazi unamuona kama choo basi wewe ni kiazi, mtu mwenye akili timamu na anayewapenda watoto wake hawezi kuwaacha chooni.
(2) Unamnyima binti wa kazi chakula, lakini pia humruhusu kukaa meza moja na wewe, kwamba kuna chakula cha binti wa kazi na chakula chakwenu. Hapa kuna mambo mawili, hivi utakulaje chakula ulichopikiwa na mtu ambaye yeye haruhusiwi kula? Akikuwekea sumu, labda achana na sumu, akakuwekea madawa yao ya kienyeji huko kwao na ujinga ujinga mwingi. Kila siku unapata malaana na magundu, watoto kila siku wanaume hujui hata wanaumwa nini?
(3) Jambo jingine ni kwamba wewe upo kazini, binti huyo unayemnyanyasa unamuacha na mwanao, yeye hujampa chakula ila umeacha cha mtoto. Haki ya nani maisha yalivyomatamu, anakichukua na kukila chote mwanao anapikiwa liuji la sembe hapo. Kuna yale maziwa ya mtoto yale ya kopo, kila siku yanaisha unasema mtoto anakula kumbe binti anakula. Sasa afanye nini kama yeye hali vizuri, hata si ujanja wala nini unakomoa wanao!
(4) Najua ushaanza kusema, “Mimi hawa mabinti wa kazi siwamini nimeweka kamera kwangu!” Najua umeweka na kuna wakati mwingine zinasaidia. Ila tatzo mnadhani kuwa hawa mabinti hawana akili kabisa, mnaona kwakua wanafanya kazi za ndani labda ni vilaza. Hapana, wanajua, wanaongea, wanasikia kuwa siku hizi kuna kamera. Wanajua unaweka sebulani, chumbani kwa mtoto na jikoni. Huko nnje wanajua hamna kitu, utahanmgaika kuangalia wee unaona mtoto yuko sawa kumbe anabemendewa nnje.
Najua huwezi kumlinda mwanao kwa asilimia mia, ni kazi ya Mungu hiyo, ila hembu fanya na wewe majukumu yako. Acha kumrahisishia binti wa kazi kazi ya kumtesa mwanao. Unavyomnyanyasa unamtengenezea roho mbaya, kisasai, hawezi kukupiga wewe lakini mwanao anaweza kumfanya chochote.
Ila ukimlea vizuri basi hatakama ana roho mbaya sana na Mungu nayeye atakulinda na wakati mwingine anaona na aibu. Kamsahara kenyewe elfu 30 lakini unamnyanyasa kana kwamba bila wewe familia yake yote inakufa! Ndugu yangu maisha haya nikusaidiana acha mdomo!
No comments:
Post a Comment