Mwanaume nisikilize nikwambie ukweli ambao utakuuma lakini utakusaidia - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanaume nisikilize nikwambie ukweli ambao utakuuma lakini utakusaidia


Image may contain: 1 person, standing, wedding, suit and outdoor
Mwanaume nisikilize nikwambie ukweli ambao utakuuma lakini utakusaidia kuepuka matatizo yatakayokupata mbele ya safari yako baada ya kuachana na Mwanamke uliyezaa nae ama Mkeo.
Usimuache wala kumtesa Mwanamke anayekupenda kwa kufanya hivyo utakuwa UMEIKOMBOA JINSIA YAKO YA KIUME kwa kuwafanya wanaume wasiteswe na wanawake, Asilimia kubwa ya MATESO wanayopitia wanaume kwa wanawake zao yamesababishwa na wanaume wenzao, Hakuna Mwanaume anaweza kumtesa Mwanamke kwa MAUMIVU alopewa na Mwanamke mwingine, Kwa sababu wanaume by nature hawajui KUPENDA ila wanaujua KUMEZA MATE😅😅
Kumekuwa na hali mbaya kwenye MAHUSIANO/NDOA za sasa na ukifuatilia unabaini kwamba chanzo kikuu ni Mwanaume, Na nilivyofuatilia nimegundua kwamba;
 WANAWAKE KUUMIZWA NA MWANAUME WA PENDO LAKE.
Kwamba Mwanaume anapomuumiza Mwanamke aliyempenda tafsiri yake ni kwamba HAKUNA MWANAUME ATAONA FURAHA KWA MWANAMKE HUYO kwa hiyo chanzo kinakuwa;
 TATIZO ANALOPATA MWANAUME KWENYE MAHUSIANO/NDOA YAKE LIMESABABISHWA NA MWANAUME MWENZIE KWA SABABU MWANAMKE HUYO PAMOJA NA KUISHI NA WEWE LAKINI UPENDO WAKE UPO KWA MWINGINE JAPO ALIMUACHA.
Hivyo Kuna haja ya wanaume kukaa chini na kupeana Elimu ya namna ambavyo wanatakiwa kusaidizana kwenye UMILIKAJI WA MWANAMKE.
Mwanaume niamini, Mwanamke yeyote ambaye aliishakuwa kwenye MAHUSAIANO ukimpata asikudanganye kwamba HAKUMPENDA MWANAUME YULE hizo ni swaga tu, Hakumpenda vipi na aliweza kumvulia nguo zake? Hakuna kitu kigumu kwa Mwanamke kama kumvulia nguo mwanaume, Maana hata KAHABA pamoja na KUPENDA pesa lakini akimpenda Mwanaume anaweza kumpa BURE😅😅😅
Mwanamke bwana humpenda Mwanaume mmoja kwa hiyo usijidai sanaaaaa pengine wewe unapoza MAUMIVU ya kuachwa au migogoro anayopitia kwenye Mahusiano ama ndoa yake, Mwanamke ili awe na AMANI MAISHANI MWAKE NI MPAKA YULE ALIYEKO KWENYE MTIMA WAKE AMPE UPENDO vinginevyo Wanaume wengine mtapewa kazi ya KUTULIZA KITI AKIPANDA lakini pia kumfariji kipindi kigumu atakachokuwa anapitia na siku yule ampendaye akionyesha kutaka MARIDHIANO hata kama ulikuwa unampa MAHABA YA KUMZIMISHA kwamba ili azinduke mpaka ndoo mbili za maji UTAONEKANA BOYA TU😅😅
Kwa maana hiyo;
"ENYI WAUME WAPENDENI WAKE ZENU ILI WASIJE KUASI WAKAENDA KUTESA WANAUME WENZENU"
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz