MWANAMKE! YAJUE MAMBO YANAYOWAKERA SANA WANAUME KWENYE NDOA - EDUSPORTSTZ

Latest

MWANAMKE! YAJUE MAMBO YANAYOWAKERA SANA WANAUME KWENYE NDOA

🏵🏵 _Wanandoa wengi huangukia katika migogoro midogo na isiyo na maana kwa sababu ya kutochunga mambo yanayowakera wenza wao. Mizozo hiyo inapoendelea huibua matatizo makubwa ambayo inakuwa vigumu kujikwamua._
......🏵🏵 _Katika kukomesha mizozo hiyo, mwanamke anatakiwa kujiepusha na kufanya mambo yafuatayo kwa kadiri iwezekanavyo na kutoyakaribia maeneo haya nyeti ambayo huwakera wanaume wengi:-_
*1 . KUWAAMBIA WATU MATATIZO BINAFSI:* ......🏵🏵 _Unaweza ukawa unazungumza na marafiki zako kuhusu baadhi ya mambo yaliyofanywa na mumeo, lakini kufichua baadhi ya siri ambazo mumeo amekupatia kwa kukuamini ni jambo hatari sana, na unatakiwa kutojaribu kufanya hivyo kwa sababu ya unyeti wake; mwanaume anapenda mkewe awe hazina ya siri zake na mshauri wake katika mambo yake yote. Hivyo, jitahidi sana kuficha na kutunza siri za mumeo, usizitangaze...._
*2. KUMSEMA VIBAYA MAMA YAKE:* ......🏵🏵 _Mama anaendelea kuwa mwanamke namba 1 katika maisha ya wanaume wengi, hivyo kutolikaribia eneo hili itayafanya maisha yako kuwa maridhawa...._
*3. KUNG’ANG’ANIA MABADILIKO YA MWENZA:* ......🏵🏵 _Wanaume wengi wanaamini kuwa wanawake hufanya kazi ya kuwabadilisha wenza wao kuwa kama wanyama wanaofugwa kwa kuwasukuma wafanye kazi na mambo wasiyoyapenda au wasiyoyataka kabisa. Hili ni eneo nyeti sana katika ndoa hasa pale mke anapomlinganisha mume na watu wengine. Iwapo unataka kumuelekeza mumeo kufanya jambo fulani usimlinganishe na watu wengine, mshauri kwa njia nyingine. Kuamiliana naye kwa namna hii kunamfanya ahisi kuwa unampa changamoto...._
*4. MALEZI YA WATOTO:* ......🏵🏵 _Wakati fulani wanandoa huzozana kwa sababu ya suala la malezi ya watoto. Mke anaweza kuhisi kuwa mume anamlea mtoto na kumfundisha baadhi ya mambo kwa njia isiyofaa. Usimkataze tu kumlea mtoto kwa njia anayeoitaka, lakini zungumza naye vizuri kuhusu mambo anayotakiwa kumfundisha na yale ambayo mtoto hatakiwi kujifunza kwa umri wake...._
*5 . KUMUACHA PEKE YAKE*: ......🏵🏵 _Kutoka pamoja na marafiki zako kwa muda mrefu na kumuacha mumeo nyumbani kwa kipindi kirefu inaweza kumkera mumeo._ ......🏵🏵 _Vivyo hivyo, iwapo hutamtilia manani mumeo na badala yake ukawa ni mtu wa kuangalia televisheni peke yako, inamfanya mume ahisi kuwa ni mtu aliyetelekezwa na asiyepewa umuhimu...._
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz