MAPENZI KATI YA WAWILI NI KAMA MELI, IKIJAA MIZIGO(MAUMIVU, VISA NA USALITI) HAIKAWII KUZAMA. - EDUSPORTSTZ

Latest

MAPENZI KATI YA WAWILI NI KAMA MELI, IKIJAA MIZIGO(MAUMIVU, VISA NA USALITI) HAIKAWII KUZAMA.

Image may contain: 1 person

Hata punda akibeba Mizigo ipo siku anachoka na kugoma kabisa kwenda hata umchape viboko 1000, hivyo ndivyo yalivyo mapenzi, moyo uliopenda kwa dhati ukiambulia maumivu yasiyo na kikomo hufikia kiwango cha mwisho na kusema SASA BASI, YATOSHA BORA NIENDE. Anaekupenda kwa dhati huenda ukamuona mdhaifu sana kwako kumbe la hasha yeye sio mdhaifu hata kidogo bali ni ule upendo wake kwako ambao ni mwingi mno kiasi ambacho kimemfanya kujishusha kwako na kukupa nafasi ya kuitawala akili yake. Amekufa ameoza kwako haoni mwingine yaani hata akiangalia picha yako tu anatetemeka na kulegea kwa msisimko, si mapepo au bangi, la hasha ni upendo tu, Umemteka ipasavyo. Sasa je! Kwa nini usimpe thamani yake??!!!!!!!!!!.....

Wanadamu wote wana tabia ya KUPENDA ila ni wachache wenye tabia ya KUPENDA KWA DHATI, usiichezee nafasi ya kupendwa kwa dhati uliyoipata kwa huyo uliye nae kwa kudhani kuwa hata mkiachana utapata mwingine La hasha hakika waeza achana nae ukajajutia maisha yako yote yaliyobaki, utakutana na wababaishaji wenzio wasiojua kupenda kwa dhati hapo ndipo utapokiona cha mtema kuni, utaisoma namba utaumizwa, utasalitiwa, utanyanyaswa mwishowe utajuta na kumkumbuka yule uliyemuacha ukidhani alikua mdhaifu. Iwapo hujui kupenda, jifunze kwa anaekupenda, MPENDE usimdharau.

Utamu wa ndoa/mapenzi ni kupendana na sio kujipendekeza, Ulimpenda mwenyewe ukamchagua moyoni mwako ukiamini yeye ndio chaguo lako sasa iweje leo umuone HAFAI au ulimchagua huku umefumba macho? ACHA ULIMBUKENI tulia na wako mheshimu jitahidi kum HANDLE aishi kwa aman, furaha itawale kati yenu hakika hutokaa umuone MBAYA, mshike usimuache maana wapo wanaommezea mate wakimpata maumivu yatahamia kwako ujutie bure.

Imepenya... Haijapenyaaaaa???!!!!!

Kama ndio comment "IMEPENYA" kisha share na marafiki twende sawa

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz