MAHUSIANO/NDOA NI KAMA MAISHA YA GARI KADIRI LINAVYOTUMIKA NDIVYO LINAVYOWEZA KUHITAJI MATENGENEZO: - EDUSPORTSTZ

Latest

MAHUSIANO/NDOA NI KAMA MAISHA YA GARI KADIRI LINAVYOTUMIKA NDIVYO LINAVYOWEZA KUHITAJI MATENGENEZO:

Image may contain: 1 person, sky, outdoor, water and nature

Watu wengi hawajui kwamba GARI hata kama ni jipya Yaani ZERO kilometre Kuna wakati litazeeka, Issue sio kuzeeka bali issue ni namna ambavyo UNALITHAMINI GARI HILO maana yake kila wakati utahitaji kuliweka katika UIMARA.
Ndivyo Mahusiano na ndoa zinavyotakiwa kutunzwa na kuboreshwa kadiri siku zinavyosogea, Mapungufu kila mmoja na vile alivyojaaliwa, Kwa sababu aliyetuumba alijua kwamba HAKUNA ALIYE MKAMILIFU bali kupitia udhaifu tunaweza kubadilika na kuwa WAAMINIFU.
Mwanzo wa Mahusiano/Ndoa mara zote ni UPYA WA PENZI kwa namna yoyote ile kila mmoja hujaribu kumfanya nwenzie kuhisi yupo mahala salama, Ndo maana mfano wangu nikauweka kwenye GARI JIPYA kwa namna yoyote Kuna ulazima wa kuhakikisha THAMANI YA PENZI LENU HAICHUJI japo ni kweli mmekuwa na MIGOGORO ya hapa na pale, Hizo ni kama service za Gari kwamba Kuna wakati lazima umwage oil na kubadili filter kwa utunzaji wa engine yako, Kwa sababu UNAAMINI UNAPENDWA NDO USIPAMBANE KUMFANYA MWENZIO AJIONE NI WA THAMANI KWAKO?
Hamuwezi kufika rafiki yangu, Na kama ndo tabia yako kujiona wa GHARAMA KULIKO MWENZIO eti yeye ndiye kutwa kukuonyesha upendo na kujinyenyekeza kwako NIAMINI HATA UKIMZAA WA KWAKO ATAKUACHA Kwani UPENDO WA KWELI haunaga hayo mambo ya kujihesabia haki bali ni wenye kuitafuta AMANI kila wakati, Leo utajiona wa gharama lakini niamini kuna wakati UTAKUWA WA KAWAIDA SANA na hapo ndipo utatamani japo Mtu wa kukupa FARAJA wala hutamuona, Jenga mshikamano kwenye Mahusiano/NDOA yako kwa ajili ya kesho, Leo tayari upo nae lakini kesho hujui atakuwa wapi.
Mtu aliyekupenda na akabaini UPENDO wake kwako hujaupa kipaumbele mara nyingi huvunjika MOYO wala asitake kuwa nawe karibu, Wakati ule atakuwa ameondoka ndipo THAMANI YAKE ITAJULIKANA kama sio leo ni baada ya wewe KUTANGA NA NJIA ukimtafuta wa kufanana nae na ukamkosa.
PURE HEART haipatikani kwa kumtafuta MBADALA ni wakati wako kujutia kwamba ALIYEKUPENDA UMEMPOTEZA.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz