LEO NGOJA NIZUNGUMZIE MIGOGORO KATIKA NDOA - EDUSPORTSTZ

Latest

LEO NGOJA NIZUNGUMZIE MIGOGORO KATIKA NDOA


Kama upo kwenye ndoa na upo kwenye tatizo kubwa, shida au mgogoro wowote na unajisikia kama ni wewe mwenyewe tu mwenye Matatizo ya ndoa, ukweli haupo mwenyewe kwa sababu kutokuwa na Matatizo hakufanyi ndoa kuwa imara bali ndoa huwa imara kwa sababu wanandoa wanajua jinsi ya kupambana na Matatizo kwa pamoja vizuri❤️
❤️Ndoa imara na zenye afya zinajua jinsi ya kupambana na hali ngumu.
Ni kawaida kila ndoa kukutana na mambo magumu katika safari ya maisha duniani.
Wakati mnaendelea na mahusiano iwe uchumba au ndoa mnaweza kukutana na tuta kubwa la ugonjwa, kuachishwa kazi, kupoteza nyumba, kifo cha mmoja katika familia yenu kama vile wazazi, biashara kuyumba kabisa au kufirisika, hapo utafanyeje
Tumesikia mara nyingi sana watu wakiwakimbia Wake zao au Waume zao pale moja ya hayo linapotokea❤️
❤️Ukweli ni kwamba huwezi kujua ndoa yako au uchumba wako ni imara kiasi gani hadi pale utakapojaribiwa❤️
❤️Matatizo yakitokea mara nyingi huweza kuvunja mahusiano vipande vipande mume huku na mke huko au wachumba kila mmoja kuachana na mwezake.
Lakini habari njema ni kwamba, wanandoa au wachumba ambao wanaweza kupita katika ugumu wowote pamoja kwa kushikamana kama super glue huwa na mahusiano imara yaliyoyoshikamana kwa nguvu za ajabu na kuwa na upendo imara kuliko mwanzo❤️
❤️Wengi hujiuliza kwa nini hili litokee kwetu tu
❤️Kwa nini Mungu amenitupa kiasi hiki
❤️Ndoa si kunywa soda kila siku ukipata kiu, si kuwa na pesa kila siku, ndoa ni kazi, kazi inayohitaji kujitoa, hata hivyo matokeo ya kushirikiana pamoja hasa wakati wa shida kwa kushikamana bila kujali ugumu unaotokea ndoa huwa imara na yenye afya ya ajabu❤️
❤️Wengine likitokea tatizo kwenye ndoa au uchumba solution ni kuacha na kutafuta mwingine, huo ni ujinga, kila binadamu ana Matatizo yake mapya kabisa na ovyo kabisa❤️
❤️Jaribu kufikiria kwa nini ulimkubali na kuona anakufaa❤️




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz