KWANINI MAPENZI YANASHAMIRI SANA KIPINDI FULANI TU.. - EDUSPORTSTZ

Latest

KWANINI MAPENZI YANASHAMIRI SANA KIPINDI FULANI TU..

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing, shoes and indoor

KWANINI MAPENZI YANASHAMIRI WAWILI WANAPOPEANA NYAKATI NZURI, ZAWADI, NA KUTOKA PAMOJA?
Wanaume wengi wamekuwa na tabia za kukubari outing na wapenzi wao pindi tu wanapokuwa wanawatongoza, Mwanaume yupo tayari hata kutembea na mwanamke kwenye MALL nia na madhumuni amfurahishe na kumjenga Mwanamke kwa maana ya UPENDO! Mwanaume yupo tayari kusave pesa ili amnunulie mpenzi wake zawadi, chakula kizuri, na kuna muda anatamani kumtembeza kila mahala KOSA NI PALE TU NGUO ZIKITOLEWA KWENYE MWILI lol👌
Wahenga walipata kunena "MBIO ZA SAKAFUNI SIKU ZOTE HUISHIA UKINGONI"
Muda mwingine Wanawake mnasababisha hali ya ninyi kudanganywa Yaani ukakutana na Mwanaume unaonyesha madhaifu yako kwamba UNAPENDA VITU FULANI FULANI... Dadaangu nikukumbushe WANAUME HUWINDA MASAA YOTE WEWE HATA KAMA UKO NAE UNAJUA NI WA KWAKO UJUE AKIPATA UPENYO ANAWEZA KUMTONGOZA MWANAMKE MWINGINE MBELE YAKO😂
Mahusiano, Ndoa ni maudhui ya neno MAPENZI👨‍❤‍👨
Sasa Basi epuka sana kuonyesha udhaifu wako kwa Mwanaume, Wanaume wanatabia za kusoma madhaifu na akibaini wewe ni mtu wa aina gani ANAKUPELEKEA KWENYE UDHAIFU WAKO ILI UJIONE UNAPENDWA na kumbe wewe ni boya tu yupo ambaye ni kiboko yake💃
Sikutukani nakwambia ili ujitambue, Napenda sana nikiona mtoto wakike akiwa kwenye MAHUSIANO matulivu Kwani mara nyingi HUNAWIRI NA KUWA MWENYE FURAHA NA AMANI MUDA WOTE! Haina maana zawadi, outing zilingane na wengine NOOOO🙋🏻‍♂
Tunaweza kuwa na outing pamoja na kununuliana zawadi kulingana na nafasi yetu, Na hata hao wenye uwezo mkubwa wanaotuzidi na wao wanazidiwa na wenye misuri zaidi yao, Kikubwa TULITUNZE PENZI LETU KWA KUPEANA FURAHA MUDA WOTE... Hayo ndo maisha, Lakini mwanzo mwa mwezi mpaka mwisho wake HUJANUNULIWA HATA MAFUTA YA KUPAKA KISA UNAKAZI NAWE UNAJIONA UNA MUME? Wajibu wa Mwanaume ni kupambania kumtunza Mwanamke wake, Ukiona Mwanaume hamtunzi mwanamke wake na ukifuatilia nyendo zake unagundua ni mzinzi ujue HUYO SIO MUME bali anatajwa kwa jinsia yake kwamba ni MWANAUME😂
Mjenzi wa PENZI NI MWANAMKE... Mtunzaji wa penzi ni MWANAUME! Maana yake kila Mwanaume ajitahidi kumpa vitu mkewe hata kama ni vidogo vidogo but VINAUJENGA MOYO WA MWANAMKE KUJIAMINI KWAMBA YUPO MAHALA SALAMA💃
Kwanini Unadhani wanawake wana-cheat? Majibu mafupi sana "ANAMPENDA MUMEWE LAKINI MWANAUME WAKE HAJUI NAMNA YA KUMFURAHISHA HAIJARISHI ANA UWEZO KIASI GANI LAKINI MWANAMKE ANAJIKUTA ANAANGUKIA PENZI NA MWANAUME ASIYE NA UWEZO ILA TU KAJAMAA KANAJUA KUBEBA HATA CHOCOLATES"
Mwanamke anapenda kupewa hata kama anauwezo kuliko anaempa INA SOUND SANA MOYONI NA AKILINI MWA MWANAMKE aonapo anakumbukwa na mwenza wake japo hata hajakipenda kitu hicho but ukiisha nunua ukampa ATAKIPA VALUE KUBWA💪🏽
Mimi Elista nimesema ila Ukiona nakuhadaa potezea tu Kwani sio lazima ufuate yangu.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria😎
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz