KUACHANA SI SULUHISHO. - EDUSPORTSTZ

Latest

KUACHANA SI SULUHISHO.


Wewe ambaye umeoa au kuolewa na upo
unafikiria kuachana na mwenzi wako.
Fikiria upya uamuzi wako.
Fikiria hao watoto mlionao, Fikiria
nyakati zote nzuri mlizokuwa nazo pamoja
kama mke na mume, Fikiria sehemu
tofauti ambazo mlitembelea pamoja,
marafiki wazuri mliokuwa nao wote wawili
kama mke na mume.
Iepuke talaka kwa gharama zote, sababu
zinazokufanya uamue kuachana na huyo
mume wako au mke wako zinaweza kuwa
ndizo zitakazokuwa sababu mara nyingine
tena mbele ya safari kama utaamua
kuoa au kuolewa tena.
Sasa unaachana na Jimmy kwa kuwa
umechoka na tabia zake za kulewa sana
pombe, au kukutaka sex mara nne kwa
siku na next time unaweza kujikuta
unaachana na John kwa kuwa anakupiga
mingumi usiku kucha na yeye sex kwa
mwaka mara moja.
Inawezekana unataka kuachana na mary
kwa sababu ni msumbufu na anakusema
hata kwa vitu vidogo, hata hivyo
unaweza kujikuta unaacha na Joyce
baadae kwa sababu si mwaminifu katika
fedha.
Sasa utaishia wapi na hiyo project ya
kuachana na kila unayeoana naye?
Ukiangalia kwa makini kinachobadilika ni
tabia na mhusika tu ila wote ni binadamu
na binadamu asiye na kasoro bado
hajazaliwa hadi leo.
Maisha ni matamu sana kiasi cha
kuyapoteza kwa kupeana talaka.
Wanaume wote duniani wanafanana pia
wanawake wote duniani wanafanana , na
sote ni binadamu.
Wapo wanandoa ni wazembe kiasi
ambacho huacha kutumia kila
alichonacho kuhakikisha ndoa inarudi
kwenye mstari, kukimbilia talaka si jibu
bali ni kusukuma tatizo mbele na matokeo
yake utakuja kukutana nalo tena mbele
ya safari.
Hata kama kuna mtu amekuahidi kwamba
ukiachana na huyo uliyenaye basi yeye
atakufanya uwe mtu mwenye furaha,
hatakuumiza wala kukuacha, ni mwongo
na anakudanganya kwani katoka sayari
gani na binadamu gani.
Anaonekana anakufaa kwa kuwa huishi
naye ukianza kuishi naye utajikuta
umeruka mikojo.
Jiulize mwenyewe upya.
Hivi kweli nimetumia uwezo kiasi gani
kuhakikisha mwenzi wangu anajua namna
tunahitaji kuirudisha ndoa yetu kwenye
mapenzi upya kama tulivyoahidiana siku
tunaoana?
Je, ni kweli nimefanya kila
linalowezekana kusamehe na kusahau?
Je, ni kweli tunataka kuachana na
kupeana talaka kwa sababu za msingi?
Kabla ya kuwasiliana na ndugu zako,
rafiki zako, washauri wako, wanasheria
au wachungaji wako Jaribu kukaa
mwenyewe, na mwenzako kujadili upya na
kwa upendo namna ya kutatua tatizo
lenu na hakuna anayejua shida ya ndoa
yako isipokuwa wewe na mwenzi wako.
Usifanye uamuzi wa kuachana kwa
haraka ukiamini unaingia kwenye uhuru.
Dawa ya kuachana au talaka ni
kusamehe bila masharti.

Mthamini mwenza wako kama unavyojidhamini wewe.
Jambo ambalo hupendi kutendewa, basi nawe pia usimtendee mwenza wako.
Yale ambayo wapenda utendewe na mwenza wako, uwe wa kwanza kuyatenda kwa mwenza wako.
ASANTE




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz